Uzidishaji
(Elekezwa kutoka Dharuba)
Katika hisabati, uzidishaji (kwa Kiingereza: multiplication) ni mojawapo kati ya vitendaji vinne vya hesabu(pamoja na ujumlishaji, utoaji na ugawanyaji). Uzidishaji ni kinyume cha ugawanyaji. Alama ya uzidishaji ni ×.[1][2]
Kwa usahihi, uzidishaji ni tendo la kujumlisha namba fulani mara kadhaa. Kwa mfano:
.
Katika mlinganyo huu, 3 ni kizidishi, 4 ni kizidishio na 12 ni zao. Kizidishi na kizidishio ni vigawo vya zao. Hata hivyo, mpangilio wa kizidishi na kizidishio haubadilishi zao. Yaani:
.
Kanuni hii hujulikana kama tabia ya mabadiliko ya kuzidisha.
Marejeo
hariri- ↑ Hisabati: Kitabu cha Mwanafunzi: Darasa la Tatu (tol. la 2). Taasisi ya Elimu Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-04-18.
- ↑ Kinyondo, Abel. Mazoezi ya hisabati kwa kadi. University of Dar es Salaam Press.
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uzidishaji kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |