Dol Kumari Karki (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Tara Devi; 15 Januari 1946 - 23 Januari 2006) alikuwa mwimbaji kutoka nchini Nepal. Anajulikana kama "Nightingale wa Nepal" kwa kuwa na nyimbo zaidi ya 4,000 wakati wa uhai wake. Muziki wake mwingi uligusia mada za uzalendo na upendo.[1][2][3]

Maisha ya awali

hariri

Alizaliwa mwaka wa 1946, katika kitongoji cha Indra Chowk huko Kathmandu, Nepal na wazazi wake Krishna Bahadur Karki na Radha Devi Karki. Tara Devi alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba na kurekodi nyimbo 4000 katika kazi yake ya kuimba kwa miaka 40. Alijihusisha na kuimba vipindi vya watoto katika redio za Nepal. Aliweza kwenda na kazi yake ya muziki pamoja na masomo yake hadi alipomaliza elimu yake katika Muziki.

Marejeo

hariri
  1. "Swar Kinnari Tara Devi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-25. Iliwekwa mnamo 2023-03-30.
  2. Tara Devi MP3 Songs
  3. Nepali Singer Tara Devi Dies at 60 Archived 7 Februari 2006 at the Wayback Machine. OhMyNews – 23 January 2006
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dol Kumari Karki kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.