Domobuluu
Domobuluu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Domobuluu kichwa-chekundu
Spermophaga ruficapilla | ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 3:
|
Madomobuluu (kutoka Kiing.: bluebill) ni ndege wadogo wa jenasi Spermophaga katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Ndege hawa ni baina ya wakubwa kabisa wa familia hii na wana domo fupi na nene sana. Wanafanana na wabanjambegu lakini domo lao ni buluu lenye ncha nyekundu. Kidari ni chekundu, mabawa na mkia ni nyeusi au kahawia na tumbo ni jeusi au kahawia lenye madoa meupe. Hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-4.
Spishi
hariri- Spermophaga haematina, Domobuluu Magharibi (Western Bluebill)
- Spermophaga poliogenys, Domobuluu wa Grant (Grant's Bluebill)
- Spermophaga ruficapilla, Domobuluu Kichwa-chekundu (Red-headed Bluebill)
Picha
hariri-
Domobuluu magharibi