Mbegu ni sehemu ya tunda la mmea inayoweza kuendelea kuwa mmea mpya. Mbegu ni njia ya kuzaliana kwa mimea mingi zinazoitwa kwa njia ya kibiolojia spermatophytina. Mbegu inaanzishwa ndani ya ua la mmea inaendelea kukua. Kuna mbegu ndogo sana ambazo ni vigumu kuona kwa jicho na mbegu kubwa kama nazi.

Mbegu za alizeti zimekauka lakini zinahitaji tu maji, halijoto ya kufaa na mwanga ili kuanzisha mmea mpya
Muundo wa ndani ya mbegu: a)ganda la mbegu b) lishe (endosperm) c) cotyledon au chanzo cha jani d) hypocotyledon au chanzo cha mzizi

Sehemu za mbegu hariri

Huwa ndani yake na sehemu tatu

  • ganda la nje au testa
  • kitoto cha mmea yaani sehemu yenye chanzo cha majani na mizizi.
  • lishe ya kitoto cha mmea au "endosperm" ambayo ni hasa akiba ya wanga na sukari, mara nyingi pia protini na mafuta. Akiba hii inalisha mmea changa hadi imekuza mizizi na majani mabichi madogo inayoweza kuanza kazi ya usanisinuru.

Kulala kwa mbegu hariri

Uwezo wa pekee wa mbegu za mimea tofauti na mimba ya wanyama ni ya kwamba kitoto kinaandaliwa ndani ya una lakini kinaacha kukua na kukauka. Katika hali kavu inaweza kukaa kwa muda, na mbegu kadhaa zimejulikana zilikaa miaka hata karne zikaweza kuchipuka hata baada ya muda mrefu.

Uwingi wa mbegu hariri

Mimea inatofautiana sana kuhusu idadi za mbegu zinazoweza kutolewa. Lakini hata mimea yenye uwezo wa kutoa mbegu nyingi hazitoi kila mwaka; hii inategemea pia na hali ya hewa (ukame na baridi), magonjwa ya mimea na wadudu. Kwa mfano wataalamu walitazama sehemu ya msitu wa misonobari kwa kipindi cha miaka 20 wakaona ya kwamba mavuno ya mbegu yalikuwa kati ya 0 na milioni 5 za mbegu kwa hektari moja. Katika miaka sita mebgu zilitokea kwa wingi sana, katika miaka mitano chache sana, na miaka kumi miti ilikuwa na kiasi kizuri cha mbegu.

Mbegu na chakula hariri

Mbegu huwa kati ya vyakula muhimu sana kwa wanadamu. Nafaka zote ni mbegu za aina za manyasi na kuwa chanzo kikii cha wanga kwa binadamu. Mbegu kama alizeti na jozi nyingi ni chanzo cha mafuta na protini.


 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: