Doreen Kessy
Doreen Kessy ni mkuu wa operesheni katika kampuni ya Ubongo, inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa njia ya katuni.[1][2]
Doreen Kessy | |
Kessy akiwa katika Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kazi yake | Mwanaharakati wa elimu |
Doreen pamoja na wenzake watano, waasisi wa kampuni ya ubongo, waliamua kuanzisha ubongo ili kutoa mchango wao katika kupunguza tatizo la ukosefu au ueneaji wa elimu kwa watoto barani Afrika.[3] Wanaamini kuwa kwa kutumia katuni hizi zitatoa mchango mkubwa katika kuwaelewesha watoto hivyo kuwapunguzia kazi kubwa walimu.[4]
Inakadiriwa kuwa familia 6.4 milioni katika nchi 31 Afrika wanatazama na kujifunza kutokana na Katuni za Ubongo kids kila wiki. [5]
Elimu
haririDoreen ana shahada ya uzamili ya biashara na utawala pia ana shahada ya kimataifa ya biashara na uchumi kutoka katika chuo kikuu cha Liberty kilichopo Virginia marekani. [6]
Kazi
haririKabla ya kuanzisha na kufanya kazi katika kampuni ya ubongo ,Doreen aliwahi pia kufanya kazi katika mashirika ya International Justice Mission ,Wells Fargo and Smile Africa na pia aliweza kubuni programu za kupunguza umaskini,ambazo zinatumika nchini Zimbabwe na Zambia. [7]
Uanaharakati
haririNi mwanaharakati wa Elimu ,ambaye anajaribu kuleta mapinduzi katika Elimu kwa watoto wa Afrika,kufanya masomo yenye dhana kuwa ni magumu kwa kuyafundisha kwa njia ya katuini ili wanafunzi waweze kuyapenda na kuelewa kwa urahisi. .[8]
Ameshiriki pia kama mmoja wa waigizaji ,kwa kuigiza sauti ya Kiingereza ya Ngedere katika katuni za Ubongo kids. .[9]
Tuzo
haririKessy,ni miongoni mwa wavumbuzi 8 walio tunukiwa tuzo katika tuzo za Elimu zilizo kuwa zikitolewa na Umoja wa Afrika(the AU Education Innovation Prizes), Dakar, Senegal, 10 Oktoba 2018.[10]
Marejeo
hariri- ↑ http://www.sheroes.co.tz/sheroes.html Archived 8 Machi 2019 at the Wayback Machine. iliangaliwa tar 7 March 2019
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-03-30. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ http://www.finland.or.tz/public/default.aspx?contentid=336675&contentlan=2&culture=en-US
- ↑ https://www.forbes.com/sites/ehrlichfu/2015/08/01/educating-kids-across-africa-through-a-local-cartoon-show/#1a587b6a237a
- ↑ https://www.weforum.org/agenda/2018/08/young-global-leaders-youth-day/
- ↑ https://www.crunchbase.com/person/doreen-kessy#section-overview
- ↑ https://www.crunchbase.com/person/doreen-kessy#section-overview
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-03-30. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-03-30. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
- ↑ https://au.int/en/pressreleases/20181010/ten-innovators-pitch-au-education-innovation-prizes
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Doreen Kessy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |