Dr. Tumi (jina halisi Tumisang Makweya; alizaliwa Seshego, Limpopo, Afrika Kusini, 10 Julai 1981) ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, mtunzi, na mtayarishaji wa muziki, pia ni daktari wa tiba.

Maisha na Kazi

hariri

Akiwa kwenye familia yenye malezi ya kidini, baba yake akiwa ni mchungaji na mama yake mwalimu, Dr. Tumi alipata motisha mapema kuhusiana na imani na muziki. Alijifunza kupiga kinanda akiwa mdogo, akipata hamasa kutoka kwa baba yake ambaye alimlea katika njia ya kumtumikia Mungu na kujenga kipaji chake cha muziki. Kazi yake ya muziki wa injili ilianza baada ya kushiriki kwenye shindano la Coca-Cola Popstars, ambako aliweza kufahamika kwa kipaji chake cha kuimba[1]. Dr. Tumi alipata umaarufu kupitia albamu zake kama The Gathering of Worshippers na Love On The Cross, na nyimbo zake maarufu kama No Other God na Wafika. Albamu yake ya Love and Grace ilipata tuzo ya platinum mara mbili, na ameshinda tuzo kadhaa ikiwemo Msanii Bora wa Injili na Msanii Bora wa Kiume katika SABC Crown Gospel Music Awards mwaka 2016. matamasha yake ya muziki yamevutia maelfu ya mashabiki, ikiwemo tamasha kubwa lililofanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome huko Johannesburg.

Mbali na muziki, Dr. Tumi ana shahada ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Medical University of Southern Africa (Medunsa) na anaendesha kituo chake cha tiba binafsi huko Mabopane. Ameoa mkewe Kgaogelo Makweya, ambaye pia ni meneja wake, na wana watoto watatu[2]. Dr. Tumi anajulikana kwa kuchanganya taaluma yake ya udaktari na huduma yake ya muziki wa injili, akilenga kuleta uponyaji wa kiroho na kimwili kupitia kazi zake za muziki na huduma ya afya.

Marejeo

hariri
  1. Peris Walubengo (2019-05-01). "Who is Dr Tumi? Get all the facts about your number 1 gospel artist". Briefly (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-11-06.
  2. Princess Tshegofatso (2021-01-15). "Dr Tumi Biography: Age, Songs, Net Worth, Pictures, Wife, Awards, Albums". TheCityCeleb (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-11-06.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dr. Tumi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.