Dropping Knowledge

Dropping Knowlege ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kuleta majadiliano dunia nzima kuhusu matatizo makubwa yanayomkabili mwanadamu.

Tarehe 9 Septemba 2006 shirika hili liliandaa tukio linaloitwa "Meza ya Sauti Huru" (the Table of Free Voices), ambapo watu 112 toka katika nyanja mbalimbali kama za sayansi, teknolojia, utamaduni, na sanaa hukaa pamoja na kujibu maswali 100. Maswali haya huchujwa toka katika maswali ambayo huulizwa na watu mbalimbali duniani kupitia tovuti ya shirika hili.

Majibu ya maswali haya hurekodiwa na kuandikwa na kuhifadhiwa ili kwa msingi wa baraza liitwalo "Maktaba Hai" (Living Library) ambapo ushiriki utakuwa wazi kwa mtu yeyote yule.

Kampuni ya bima ya Munich, Ujerumani, Allianz inatoa msaada wa fedha kwa shirika hili kwa miaka miwili, toka mwaka 2005 - 2007.

Maswali

hariri

Sehemu kubwa ya mradi huu unaoendeshwa na shirika la Dropping Knowledge ni maswali yanayotumwa na watu toka sehemu mbalimbali duniani kupitia tovuti yao. Shirika hili linaamini kuwa tukiuliza maswali sahihi na tukayajibu, huo utakuwa ni mwanzo wa kujenga jamii bora zaidi duniani.

Meza ya Sauti Huru (The Table of Free Voices)

hariri

Tarehe 9 Septemba 2006 watu toka katika nyanja mbalimbali duniani watakutaka August-Bebel-Platz, Berlin, mahali ambapo serikali ya Kinazi ya Ujerumani ilichoma moto vitabu mwaka 1933 ili kujibu maswali 100 yaliyochaguliwa. Maswali haya yataulizwa na kujibiwa na washiriki wote 112 kwa wakati mmoja. Kila mshiriki atakuwa na kamera mbele yake itakayorekodi jibu lake. Majibu haya baadaye yataweka kwenye Intaneti.

Maktaba Hai (Living Library)

hariri

Maktaba Hai ni baraza ambapo watu wataweza kushiriki katika mijadala itakayotokana na majibu ya maswali 100 yaliyojibiwa.

Viungo vya nje

hariri