Chogha Zanbil
Chogha Zanbil (kwa Kiajemi چغازنبيل ; kwa Kielami: Dur Untash) ni eneo la maghofu ya mji wa kifalme wa Waelami katika mkoa wa Khuzestan nchini Iran. Kitovu chake ni sehemu ya mahekalu ya mji ule, penye mnara wa zigurati ambao ni mmojawapo wa machache katika Mesopotamia nje ya Iraki. Iko takriban km 30 (mi 19) kusini mashariki mwa Susa na km 80 (mi 50) kaskazini mwa Ahvaz .
Jina
haririChoga Zanbil mara nyingi hutafsiriwa kama 'kilima cha kikapu.' [1] Ilijengwa mnamo mwaka 1250 KK na mfalme Untash-Napirisha, hasa kwa ajili ya kumtukuza mungu mkuu Inshushinak . Jina lake la asili lilikuwa Dur Untash, ambalo linamaanisha 'mji wa Untash' kwa Kiashuru, lakini kuna uwezekano kwamba watu wengi, mbali na makuhani na watumishi, waliwahi kuishi huko. Eneo la mahekalu linalindwa na kuta tatu ambazo hufafanua maeneo makuu ya 'mji'. Eneo la ndani limechukuliwa kabisa na zigurat kubwa iliyowekwa wakf kwa mungu mkuu, ambayo ilijengwa juu ya hekalu la awali na vyumba vya pembeni vilivyojengwa na Untash-Napirisha. [2]
Awali zigurat ilikuwa na msingi mwenye urefu wa mita 105 kila upande na kimo cha mita 53. Ilijengwa katika ngazi ngazi tano, na juu yake ilikaa hekalu yenyewe. Yote yalijengwa kwa kutumia matofali ya matope. Sura ya nje ilipambwa kwa matofali ya kuchoma, ambayo baadhi yake yana herufi za kikabari zinazotaja majina ya miungu katika lugha za Kielami na Kiakkadi. Kwa sasa zigurat ina kimo cha mita 24,75 pekee, amabyo ni takriban nusu ya kimo cha kiasili. Hata hivyo ni mfano bora zaidi wa zigurat ya ngazi uliohifadhiwa na hivyo imepokelewa na UNESCO . [3] Mnamo 1979, Chogha Zanbil ikawa mahali pa kwanza nchini Iran iliyoandikishwa katika Orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO .
Picha
hariri-
Zigurat ya Dur Untash
-
Zigurat ya Dur Untash, upandeambako uso ulitengenezwa kisehemu
-
Mfano wa zigurat nchini Iraki: Dur-Kurigalzu
-
Nchini Iraki: Zigurat ya Ur
-
Picha zinazolinganisha zigurat mbalimbali
-
Kifaa cha kufunga mlango; ni tofali lilikuwa na rangi ya buluu. Mwandiko wa kikabari unasema: "Ikulu ya Untash-Napirisha, Mfalme wa Elam". karne ya 13 KK, iliokowa Chogha Zanbil, Iran. Sasa British Museum, Uingereza.
Marejeo
hariri- ↑ Rohl, D: Legend: The Genesis of Civilisation, page 82. Century, 1998.
- ↑ R. Ghirshman, The Ziggurat of Tchoga-Zanbil, Scientific American, vol. 204, pp. 69–76, 1961
- ↑ "Tchogha Zanbil", UNESCO World Heritage Centre. "It is the largest ziggurat outside of Mesopotamia and the best preserved of this type of stepped pyramidal monument."
Viungo vya nje
hariri- 6,000-Year-Old Ziggurat Found Near Chogha Zanbil In Iran - 2004 Ilihifadhiwa 4 Machi 2016 kwenye Wayback Machine.
- Chogha Zanbil Ilihifadhiwa 26 Desemba 2016 kwenye Wayback Machine.
- World Heritage profile
- guide to Choga Zanbil Ilihifadhiwa 19 Aprili 2017 kwenye Wayback Machine.