Mesopotamia ni jina la kihistoria kwa mabonde ya mito Frati na Hidekeli yanayogawiwa leo kati ya nchi za Uturuki, Syria na Irak.

Ramani ya Mesopotamia

Neno limetoka katika lugha ya Kigiriki "Μεσοποταμία" kutokana na maneno asilia ya μεσο meso (kati ya) na ποταμός potamos (mto), hivyo ni "nchi kati ya mito". Mito hii ni Frati (Euphrates) na Hidekeli (Tigris).

Mesopotamia ilikuwa ya kwanza kati ya nchi zilizokuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu kwa kuanza uzalishaji, kujenga miji ya kwanza kabisa duniani, kama vile Sumeri na Babeli, kuwa na serikali na sheria, na kubuni mwandiko.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mesopotamia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.