Dutu sanisi au dutu sintetiki ni dutu zinazoundwa na binadamu kwa mbinu za kikemia kwenye maabara au viwanda, tofauti na dutu asilia kama ubao au mwamba.

Dutu sanisi hupatikana ama kwa kuiga kazi inayotekelezwa kiasili, mfano kukuza fuwele katika maabara na kuzigandaniza ili kuzalisha almasi sintetiki, ama kwa kuunganisha molekuli na kujenga polima kama aina mbalimbali za plastiki.

Malighafi katika uzalishaji wa dutu sanisi mara nyingi hupatikana kiasili kama vile mafuta ya petroli.

Elementi sintetiki ni elementi za kikemia zinazoundwa katika maabara kwa njia za kifizikia.

Tazama pia

hariri