Maabara (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: Laboratory) ni jengo au chumba maalumu kinachotumika kwa ajili ya majaribio na utafiti wa kisayansi.

Maabara ya uganga wa kansa huko Taiwan.
Maabara ya biolojia ya molekuli huko Poznan, Poland.
Benchi katika maabara ya kemia.

Kuna aina mbalimbali za maabara, mfano: maabara za biolojia, maabara za kemia, maabara za fizikia n.k.

Vilevile kuna maabara zinazotumika katika hospitali na katika majaribio mengine ya kisayansi. Kwa mfano, maabara ya biolojia ni jengo au chumba maalumu kwa ajili ya kufanyia majaribio yahusuyo viumbe hai.

Historia

hariri

Maabara za zamani katika nchi ya Uingereza zilikuwa za kutengenezea dawa. Vita vya pili vya dunia vilifanya maabara ziwe kubwa kwa minajili ya kutengenezea zana za vita za kiatomiki.

Leo maabara bado zinatumika kwa madhumuni ya kutengenezea na kujaribu dawa, kuunda zana za vita na pia kufundisha katika shule.

Sheria za maabara

hariri
 • 1. Usiingie ndani ya maabara mpaka uruhusiwe.
 • 2. Usikimbie ndani ya maabara.
 • 3. Usile kitu chochote ndani ya maabara.
 • 4. Usitumie kifaa kilichoharibika.
 • 5. Ripoti tatizo lolote litakalojitokeza.
 • 6. Usifanye kitu chochote bila ruhusa
 • 7. Osha mikono baada ya kumaliza kufanya majaribio au utafiti

Sifa za maabara

hariri
 • 1. Iwe na madirisha makubwa.
 • 2. Iwe na milango miwili inayofunguka kwa nje.
 • 3. Iwe na mfumo mzuri wa umeme.
 • 4. Iwe na vifaa vya kutosha.
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maabara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.