Efunroye Tinubu
Mwanasiasa wa Nigeria
Efunroye Tinubu (jina la kuzaliwa Ẹfúnpọ̀róyè Ọ̀ṣuntinúbú, mnamo 1810 – 1887) alikuwa mwanamke mwenye nguvu wa kabila la Wayoruba na mfanyabiashara wa utumwa katika nchi ya Nigeria kabla ya ukoloni.[1][2][3]
Alikuwa mtu wa maana kisiasa na kiuchumi jijini Lagos wakati wa utawala wa Obas (wafalme) Adele, Dosunmu, Oluwole, na Akitoye, akisaidia wafalme wawili wa mwisho kupata nguvu za kisiasa. Alikuwa ameolewa na Oba Adele na kutumia uhusiano wake kuanzisha mtandao wa biashara wenye mafanikio na wafanyabiashara wa Ulaya katika utumwa, tumbaku, chumvi, pamba, mafuta ya nazi, na silaha. Inasemekana alikuwa na watumwa zaidi ya 360 binafsi.
Tanbihi
hariri- ↑ Bonnie G. Smith (2004). Women's History in Global Perspective, Volume 3. University of California, Berkeley (University of Illinois Press). uk. 40. ISBN 9780252072345.
- ↑ "Madam Tinubu: Inside the political and business empire of a 19th century heroine", The Nation.
- ↑ Judybee (2011). Madam Tinubu: Queens of Africa. MX Publishing. ISBN 978-1-908-2185-82.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Efunroye Tinubu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |