Einigkeit und Recht und Freiheit

Einigkeit und Recht und Freiheit ("Umoja na haki na uhuru") ni maneno ya kwanza ya wimbo wa taifa la Ujerumani. Wimbo huo ulitungwa kiasili na mshairi Hoffmann von Fallersleben mwaka 1841 kama "wimbo la Wajerumani" (Lied der Deutschen) likiwa na mabeti matatu. Lakini beti ya tatu pekee inayokubaliwa kama wimbo la taifa. Muziki yake iliandikwa na Joseph Haydn.

Beti asilia ya kwanza inajulikana kutokana na chanzo chake "Ujerumani juu ya yote" (Deutschland, Deutschland über alles) lakini baada ya maarifa ya utaifa mkali katika karne ya 20 uliopeleka nchi katika vita kuu mbili Wajerumani wengi hawapendi tena beti hii hivyo haitumiki tena.

Maeneo yaliyokaliwa na Wajerumani wakati wa karne ya 19

Historia

hariri

Joseph Haydn alitunga muziki hii kwa heshima ya Kaisari Franz wa Austria na Dola Takatifu la Kiroma likawa wimbo la taifa la Austria hadi mwisho wa ufalme mwaka 1918.

Muziki latumiwa pia kwa nyimbo za kanisani katika nchi mbalimbali.

Mshairi August Heinrich Hoffman von Fallersleben alitunga shairi kwa ajili ya muziki hii mwaka 1841. Wakati huu Ujerumani iligawanyika katika madola mengi madogo. Kati ya wananchi hamu ilikuwa kubwa kuungana lakini wanasiasa katika kila sehemu hawakuona faida kuachana na hali halisi. Kwa wibo wake alitaja mipaka ya ameneo walipokaa watu waliosema Kijerumani katika madola mbalimbali, wengi ndani ya mipaka ya Shirikisho la Ujerumani lakini pia wengine nje yake. Alitaka kutamka tumaini alke wote wataunganishwa siku moja.

Baada ya vita mbili maeneo makubwa yaliyokaliwa na wasemaji wa Kijerumani wakati wa Hoffmann yako chini ya nchi nyingine na wakazi wa awali hawako tena; ama walizoea lugha nyingine au walifukuzwa hasa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kwa sababu hii majirani wa Ujerumani waliona maneno ya bei ya kwanza kwa mashaka, na Wajerumani wenyewe hawakutaka tena kuimba majina ya mito ambayao sasa ni sehemu ya mataifa mengine kwa hiyo hawatumii beti ya kwanza tena.

Katika karne ya 19 wimbo la Hoffmann lilipendwa na watu lakini halikuwa wimbo la kitaifa lililokuwa wimbo la kumsifu kaisari hadi 1918. 1922 lilitangazwa kuwa wimbo la taifa katika jamhuri ya Ujerumani; baada ya vita kuu ya pili rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani alitangaza beti ya tatu kama wimbo la taifa lakini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani walikuwa na nyimbo tofauti. Tangu 1990 beti la tatu ni wimbo la Ujerumani iliyounanika.

Maneno ya Kijerumani

hariri

Tafsiri kwa Kiswahili

hariri

Beti ya Kwanza

hariri
Deutschland, Deutschland über alles,
über alles in der Welt,
wenn es stets zu Schutz und Trutze
brüderlich zusammenhält.
Von der Maas bis an die Memel,
von der Etsch bis an den Belt,
|: Deutschland, Deutschland über alles,
über alles in der Welt! :|
Ujerumani, Ujerumani juu ya yote
juu ya yote duniani
kama muda wote kwa ulinzi
inasimama kindugu
kutoka mto Meuse (upande wa magharibi) hadi mto Neman (upande wa mashariki),
kutoka mto Adige (upande wa kusini mpakani wa Italia) hadi Belt (Bahari upande wa kaskazini /Denmark).
|: Ujerumani, Ujerumani juu ya yote
juu ya yote duniani. :|

Beti ya Pili

hariri
Deutsche Frauen, deutsche Treue,
deutscher Wein und deutscher Sang
sollen in der Welt behalten
ihren alten schönen Klang,
uns zu edler Tat begeistern
unser ganzes Leben lang. -
|: Deutsche Frauen, deutsche Treue,
deutscher Wein und deutscher Sang! :|
Wanawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,
divai ya Kijerumani na nyimbo za Kijerumani
ziendelee kuwa kote duniani
na sifa zao njema
na kutuhamasisha kutenda mema
kwa muda wa maisha yetu yote.
|: Wanawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,
Wanawake wa Kijerumani, uaminifu wa Kijerumani,

Beti ya tatu - Wimbo rasmi la Taifa la Ujerumani

hariri
Einigkeit und Recht und Freiheit
für das deutsche Vaterland!
Danach lasst uns alle streben
brüderlich mit Herz und Hand!
Einigkeit und Recht und Freiheit
sind des Glückes Unterpfand;
|: blüh im Glanze dieses Glückes,
blühe, deutsches Vaterland. :|
Umoja na haki na uhuru
kwa nchi ya Kijerumani
Huku tushikamane sisi sote
kindugu kwa moyo na mkono
Umoja na haki na uhuru
ni hakikisho la raha
|: Ustawi katika mwangaza wa raha hiyo,
Ustawi nchi yetu ya Kijerumani :|