Austria

nchi katika Ulaya ya Kati

Austria (kwa Kijerumani: Österreich) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Ucheki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi na Liechtenstein.

'Republik Österreich
Jamhuri ya Austria
Bendera ya Austria Nembo ya Austria
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: “'Land der Berge, Land am Strome
(Kijerumani kwa "Nchi ya milima, nchi ya mtoni")
Lokeshen ya Austria
Mji mkuu Vienna
48°12′ N 16°21′ E
Mji mkubwa nchini Vienna
Lugha rasmi Kijerumani 1
Serikali Jamhuri
Alexander Van der Bellen
Karl Nehammer
Uhuru
Mkataba kuhusu Austria ulianza
Tangazo la baki

27 Julai 1955
26 Oktoba 1955
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
83,871 km² (ya 115)
1.3
Idadi ya watu
 - 2022 kadirio
 - 2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9,027,999 (ya 98)
8,932,664
107.6/km² (ya 106)
Fedha Euro () 2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .at 3
Kodi ya simu +43
1 Kislovenia, Kikroatia, Kihungaria ni lugha rasmi kieneo.
2 Kabla ya 1999: Shilingi ya Austria.


Ramani ya Austria

Mji mkuu ni Vienna.

Jiografia

hariri
 
Austria:Uso wa nchi
 
Mlima Grossglockner

Eneo la nchi lina umbo ndefu na nyembamba kama kanda linaloelekea kutoka mashariki kwenda magharibi.

Sehemu kubwa ya Austria (60%) ni milima. Tambarare ziko hasa kando la mto Danubi ambao ni pia mto mkubwa. Theluthi moja ya eneo liko chini ya mita 500 juu ya usawa wa bahari. Zaidi ya 40% za nchi ni misitu. Mto Danubi unavuka sehemu kubwa ya nchi.

Milima mikubwa ya Austria inafikia kimo kati ya mita 3000 na 4000. Katika hali ya hewa ya nchi kuna theluji mwaka wote. Mlima mkubwa ni Grossglockner wenye mita 3,798, halafu Wildspitze wenye mita 3,774 juu ya UB.

Ziwa kubwa ni ziwa la Neusiedler See lililopo mpakani kwa Hungaria. Mlimani kuna maziwa mengi madogo.

Uso huo wa nchi ni msingi wa utalii ulio muhimu sana Austria. Wakati wa joto watalii wanaponda baridi ya milima; wakati wa baridi wanakuja kucheza ski.

Majimbo

hariri
Makala kuu: Majimbo ya Austria
Nafasi Jimbo Makao
makuu
Jina rasmi Wakazi Eneo (km²)
1 Vienna Vienna Wien 1,677,867 415
2 Austria Chini Sankt Pölten Niederösterreich 1,597,240 19,178
3 Austria Juu Linz Oberösterreich 1,408,165 11,982
4 Steiermark Graz Steiermark 1,205,609 16,392
5 Tirol Innsbruck Tirol 703,512 12,648
6 Karinthia Klagenfurt Kärnten 561,094 9,536
7 Salzburg Salzburg Salzburg 530,576 7,154
8 Vorarlberg Bregenz Vorarlberg 366,377 2,601
9 Burgenland Eisenstadt Burgenland 281,190 3,965

Hali halisi kuna jiji moja tu ambalo ni mji mkuu Wien (Vienna). Ulikua kama mji mkuu wa Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma na baadaye wa milki ya Austria iliyojumlisha sehemu kubwa za Ulaya ya Kusini-Mashariki.

Miji mingine mikubwa kiasi ni

Historia

hariri

Austria kama nchi ndogo jinsi ilivyo sasa imepatikana mwaka 1918 na tena tangu 1945.

Kwa muda mrefu wa historia yake Austria ilihesabiwa kama sehemu ya Ujerumani. Kwa karne nyingi watawala wake walishika cheo cha Kaisari wa Dola takatifu la Roma lililojumlisha Ujerumani wote.

Austria ilitawala pia sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki. Watawala wa Austria walishika pia vyeo vya kifalme vya nchi za Bohemia na Hungaria.

Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari Franz II alilazimishwa kujiuzulu kama Kaisari wa Ujerumani wote mwaka 1806 akabaki na cheo cha Kaisari wa Austria tu. Baada ya Napoleoni Austria ilikuwa nchi muhimu katika shirikisho la Ujerumani.

Mwaka 1866 Austria ilishindwa katika vita dhidi ya Prussia ikatoka katika siasa ya Ujerumani. Baada ya vita hiyo Kaisari Franz-Josef alipaswa kuwakubalia Wahungaria cheo sawa na Wajerumani ndani ya milki yake. Kuanzia hapo milki ilijulikana kama Austria-Hungaria

Hadi Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia Austria-Hungaria iliendelea kutawala nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na Ucheki, Slovakia, Slovenia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina, na sehemu kubwa ya Poland ya Kusini, pia sehemu zilizopo sasa katika kaskazini mwa Italia.

Mwisho wa vita dola hili lilisambaratishwa. Sehemu zake zote zikawa nchi huru. Nchi ndogo ambayo ilikaliwa na Waaustria Wajerumani ilibaki. Washindi wa vita walizuia Waaustria wasijiunge na Ujerumani, hivyo Jamhuri ya Austria ilianzishwa.

Mwaka 1938 dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler (aliyekuwa Mwaustria mwenyewe) alivamia Austria kwa jeshi lake na kuiunganisha na Ujerumani. Wakati ule sehemu kubwa ya Waaustria walikubali.

Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Austria ilirudishwa kuwa nchi ya pekee ikabaki hivyo.

Mwaka 1995 Austria ikajiunga na Umoja wa Ulaya.

Usafiri

hariri
 
Wien Westbahnhof, mbele kabisa stendi ya teksi na kituo cha kukodisha baiskeli kutoka "Citybike Wien"

Treni za masafa marefu, za kikanda na S-Bahn zinafanya kazi huko Austria. Treni za masafa marefu katika trafiki ya mchana ni "Railjet (RJ)" "Railjet Express (RJX)" "Intercity (IC)", "Eurocity (EC)" "" Westbahn (WEST) "" Regiojet (RGJ) "na katika trafiki ya usiku" Nightjet (NJ) ". Katika trafiki ya eneo hilo kuna aina za treni "Regionalexpress (REX)" "Cityjet-Express" (CJX) "na" Regionalzug (R) ". "S-Bahn" huunganisha miji mikubwa na mazingira yao.

Mabasi ya umma ya umbali mrefu huenda huko Ujerumani na nje ya nchi. Kituo kikubwa cha mabasi ya umbali mrefu ni "Vienna International Busterminal" katika wilaya ya "Erdberg" ya Vienna, vituo vingine vya mabasi ya masafa marefu na vituo ni "Busterminal Vienna", na vituo vya basi katika vituo vya gari moshi vya Linz, Salzburg, Graz na Innsbruck.

Gari/pikipiki

hariri

Barabara nyingine zinadai malipo. Stika inayoitwa "Vignette" inahitajika kwa matumizi. Hii inaweza kununuliwa katika vituo vya mafuta, katika maduka ya tumbaku na katika ofisi za posta. Bei ni 2020: Kwa magari: siku 10: € 9.40, miezi 2: 27.40, mwaka mmoja: € 91.10, kwa pikipiki: siku 10: € 5.40, miezi 2: € 13.70, mwaka mmoja: € 36.20. Kuna ada ya ziada kwenye sehemu tano za barabara kuu, inayojulikana kama ushuru maalum, hizi ni: A1, A7, A12, A14 na A26, ada hii hulipwa kwenye tovuti kwenye kituo cha ushuru.

 
Kivuko cha Vienna-Bratislava "Twin City Liner" kwenye uwanja wa Schwedenplatz kwenye Mfereji wa Danube huko Vienna

Kwa kuwa Austria ni nchi isiyokuwa na bahari wala pwani, hakuna idadi kubwa ya vivuko vinavyopatikana. "Twincityliner" ni kivuko kinachotoka Schwedenplatz huko Vienna kwenda mji mkuu wa Slovakia, Bratislava. Uunganisho zaidi wa kivuko upo kwenye ziwa Bodensee.

Uwanja wa ndege mkubwa ni "Wien-Schwechat" karibu na Vienna huko Lower Austria. Kuja kutoka Vienna inaweza kufikiwa na laini ya S7, treni za RJ na mabasi ya kuhamisha pamoja na "Treni ya Uwanja wa Ndege wa Jiji". Kuna uhusiano wa moja kwa moja kutoka Vienna hadi mabara yote. Kuna viwanja vya ndege vingine huko Linz, Salzburg, Klagenfurt, Graz na Innsbruck.

Kutembea / kuendesha baiskeli

hariri

Hasa katika miji mikubwa ya Vienna, Linz, Salzburg, Graz, Klagenfurt na Innsbruck, baiskeli na kutembea ni chaguzi nzuri za uhamaji. Hasa huko Vienna kuna mtandao mnene wa njia za baiskeli, vifaa vingi vya maegesho ya baiskeli na vituo vya kukodisha baiskeli. Wakati wa baiskeli za maegesho, hata hivyo, unapaswa kuzingatia ulinzi wa wizi, kuwa mwangalifu dhidi ya wezi wa baiskeli!

Wakazi

hariri

Kati ya wakazi, Waaustria wenyewe ni 75.6%. Wao huzungumza Kijerumani ambacho ni pia lugha rasmi. Mpakani upande wa kusini na mashariki kuna pia wasemaji wa Kikroatia, Kislovenia na Kihungaria. Lugha hizi zina cheo rasmi kieneo au kitarafa.

Kwa jumla lahaja na utamaduni hufanana katika mengi na ile ya Wabavaria katika jimbo la jirani la Ujerumani. Kama huko wananchi wengi ni Wakatoliki (55.2%) na Wakristo wengine (9%), hasa Waorthodoksi.

Waaustria mashuhuri duniani

hariri

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya  
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Austria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.