Edinburgh
Edinburgh (kwa Kigaeli: Dùn Èideann) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa pili wa Uskoti wenye wakazi 435,790 (2005). Mji uko kwenye pwani ya mashariki ya Uskoti kwenye mdomo wa mto Forth baharini.
Boma la Edinburgh liko katikati ya mji kwenye kilima kikali.
Edinburgh imejulikana kote Ulaya kwa sababu ya sherehe yake ya maigizo inayofanyika kila mwaka na washiriki elfu kadhaa.
Historia
haririBoma lilianzishwa kabla ya karne ya 7 BK. Mji ulianza kukua kando la boma. Mwaka 1437 umekuwa mji mkuu wa Uskoti badala ya Perth. Ilikuwa pia mahali pa kukutana kwa bunge la Uskoti liliopata jengo lake la pekee mwaka 1639. Baada ya maungano ya Uingereza na Uskoti mwaka 1707 hapakuwa tena na serikali au bunge la pekee hadi 1999 mwaka wa kurudishwa bunge na serikaliya kijimbo kwa Uskoti. Edinburgh imekuwa tena mji mkuu wa angalau wa jimbo linalojitawala katika mambo ya ndani.
Picha za Edinburgh
hariri-
Kilima cha "Kiti cha Arthur" (kwa Kiingereza "Arthur's Seat") kinavyoonekana kutoka "Kilima cha Blackford" ("Blackford Hill")
-
"New College", Chuo cha Teolojia
-
Kanisa Kuu la Mt. Giles
Watu maarufu
hariri- J. K. Rowling (*1965 - )
- James Peace (*1963 - )
- Sir Sean Connery (1930 - 2020)
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Edinburgh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |