Eneo katika elimu ya jiometria ni idadi inayoeleza ukubwa wa umbo bapa lenye upana na urefu. Kwa hiyo „eneo“ linataja ukubwa wa gimba lenye wanda mbili.

Maumbo matatu ya jiometria yenye maeneo tofauti (msambamba, pembetatu, duara)

Hii inamaanisha maumbo ya jiografia bapa kama vile mraba, mstatili na duara lakini pia uso wa gimba lenye wanda tatu kama vile mchamrembe au tufe.

Ukubwa wa eneo linapimwa kwa kuulinganisha na miraba maalumu. Katika mfumo wa vipimo sanifu vya kimataifa kizio sanifu ni mita ya mraba (inayofupishwa kwa m²). Umbo kama mviringo mwenye eneo la 3 una eneo sawa na miraba mitatu ya aina hii.

Matumizi ya kipimo cha eneo hariri

Makadirio ya eneo yana faida nyingi katika maisha ya kila siku. Nikitaka kupiga rangi kuta za chumba naweza kupima maeneo yote ya kuta zake. Kwa mfano chumba cha mita 3x4 na kimo cha mita 2 lina eneo la kuta zake za 28 m² (Kuta 2 zenye upana wa mita 3 x kimo mita 2 ni 2x3=6 x kimo 2 = 12m²; kuta 2 zenye upana wa mita 4 ni 2x4= 8 x kimo 2= 16 m²; 16m²+18m² = 28 m²). Nikijua hii naweza kuuliza dukani je wana rangi gani kwa ajili ya ukuta na kopo la rangi linatosha kwa mita za mraba ngapi? Wakisema 10 m ² najua nitahitaji kununua kopo 3. Katika mfano wa juu naweza kutoa eneo la mlango na madirisha labda zinatosha kopo 2 kubwa na 1 ndogo.

Vivyo hivyo naweza kukadiria kiasi cha mbolea kwa eneo la shamba na kadhalika.

 
Tetrahedroni
 
Pia ambako uso umetandazwa bapa

Makadirio ya eneo la umbo hariri

Umbo Majina Eneo  
Mraba Urefu wa upande    
Mstatili Urefu wa pande    
Pembetatu
Upande wa msingi  , kimo  , pembemraba kwa    
Duara Rediasi    

Makadirio ya eneo la uso la gimba hariri

Gimba Majina Eneo la uso  
Mchemraba Urefu wa upande    
Tetrahedroni Urefu wa upande    
Tufe
Rediasi    
Pia Rediasi ya duara la msingi  , Kimo