Eneo chini ya taji la Uingereza
Maeneo chini ya taji la Uingereza ni visiwa vidogo kadhaa karibu na Uingereza ambavyo vimekuwa chini ya wafalme wa Uingereza tangu karne nyingi lakini hazikuunganishwa na ufalme wa Uingereza.
Hivi ni Visiwa vya Mfereji wa Kiingereza (kama Jersey, Guernsey) pamoja na Isle of Man. Vyote si sehemu za Uingereza wala za Ufalme wa Muungano wa Britania pia si sehemu za Umoja wa Ulaya. Lakini si nchi huru kama nchi nyingine za Jumuiya ya Madola.
Kwa sababu mfalme au malkia wa Uingereza hatawali tena jinsi ilivyokuwa zamani hali halisi madaraka yake juu ya visiwa hivi yapo mkononi mwa serikali ya Uingereza na sheria za bunge la London zinaweza kugusia visiwa pia. Mambo ya nje kwa jumla yako upande wa serikali ya Uingereza pia maswali ya usalama na jeshi. "Taji" yaani serikali ya Uingereza kwa niaba ya malkia imewajibika pia kuhusu utaratibu wa kisheria visiwani kama matatizo yanatokea katika maswali yote yasiyomalizwa visiwani penyewe.
Raia wa visiwa wanaangaliwa kama Waingereza wakiwa Uingereza au nje. Lakini Waingereza wanatazamiwa kama watu wa nje wakija visiwani katika utaratibu wa kununua mali, nyumba au kutafuta ajira.
Bailiwick ya Guernsey
haririEneo la Guernsey laitwa "Bailiwick" ambalo ni kitengo cha kiutawala cha kale kinachofanana na wilaya. Lajumlisha visiwa vya Guernsey, Sark, Alderney, Herm na vingine vidogo. Lina bunge lake na ndani yake Sark na Alderney vina viwango mbalimbali vya kujitawala.
Guernsey hutoa pesa yake yenyewe inayotumiwa pamoja na pesa ya Kiingereza.
Ina mahakama yake na utaratibu wake kuhusu huduma za afya na kadi.
Bailiwick ya Jersey
haririWilaya hii ni kisiwa cha Jersey pamoja na visiwa vidogo visivyo na watu
Utaratibu wake hufanana na Guenrsey.
Isle of Man
haririKisiwa cha Man kimejitawala tangu mwaka 979. Kimejulikana kuwa na bunge lake tangu wakati ule. Malkia wa Uingereza ni muu wa Dola kama Mtemi wa Man. Man hutoa pesa na stempu za posta.