Ester Alexander Mahawe

Ester Alexander Mahawe ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa miaka 20152020. [1].

Ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Kigoma kuanzia mwaka 2021. Katika uteuzi uliofanyika mapema mwaka 2023 na Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amehamishiwa Wilaya ya Mbozi iliyopo Mkoa wa Songwe.

Amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wasichana wanapata elimu bora kwa ajili ya maendeleo ya wilaya na mkoa kwa ujumla.

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017