Eylem Tuncaelli
Eylem Tuncaelli ni mwanaharakati wa kisiasa kutoka Uturuki na mwenyekiti mwenza na msemaji wa chama cha Green Left Party.[1] Alikuwa pia Mwenyekiti wa zamani wa Tawi la Istanbul la Chama cha Uhandisi wa Mazingira.[2]
Biografia
haririAlizaliwa mnamo 1975 huko Istanbul. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Trakya katika fani ya Uhandisi wa Mazingira mwaka 1999 na mwaka wa 2000 alijiunga na TMMOB (Muungano wa Vyama vya Wahandisi na Wasanifu wa Kituruki). Kati ya 2004 na 2010, alijiunga kama rais wa Tawi la Istanbul la Chama cha Uhandisi wa Mazingira, na kuwa mwanachama hai. Mnamo 2012, pamoja na wengine kama Naci Sonmez, alianzisha chama cha Green Left Party.[2]
Jela
haririMnamo 9 Februari, 2018, yeye na wanachama wengine 10 walikamatwa saa 12 asubuhi, [3][4] wakishutumiwa kwa "kuzalisha uadui kati ya watu" na "propaganda kwa shirika la kigaidi". Wafungwa hao walikuwa wakipinga hatua ya jeshi la Uturuki nchini Syria. Katika mwaka huo huo, waliachiliwa, lakini hati zao za kusafiria zilichukuliwa, na kuwazuia kusafiri Kwenda nchi zingine.[2][5]
Marejeo
hariri- ↑ "Turkish Green co-chairs Eylem Tuncaelli and Naci Sönmez are released". European Greens. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-24. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Stop the leaders of the Turkish Green Party from being jailed under false charges". European Greens. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-23. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help) - ↑ "Immediate release of Turkish Green/Left Co-Chairs Eylem Tuncaelli and Naci Sonmez! - Ska Keller, MdEP". skakeller.de. 9 Februari 2018. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "[Green Gazette weekly Turkey digest:] Arrests, Nukes, and banned children's play - Yeşil Gazete". yesilgazete.org. 13 Februari 2018. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Yeşil Sol Parti Eş Sözcülerinin Pasaportlarına El Konuldu". bianet. Iliwekwa mnamo 2022-02-25.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eylem Tuncaelli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |