Fátima Djarra Sani
Fátima Djarra Sani (alizaliwa 1968) ni mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Guinea Bissau anayepinga ukeketaji wa wasichana.
Fátima Djarra Sani | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 1968 |
Nchi | Guinea Bisau |
Kazi yake | mwanaharakati wa haki za wanawake |
Maisha ya awali
haririFátima Djarra Sani alizaliwa Bissau, mji mkuu wa nchi, mwaka 1968.[1] Ni mwanaharakati dhidi ya ukeketaji wa wanawake katika nchi ya Guinea Bisau na mwakilishi wa shirika la Médecins du Monde Afrika.[2]
Kazi
haririMwaka 2008, alijiunga na Médecins du Monde, na aliendesha warsha na mafundisho mengine kuhusu hali ya wanawake katika Afrika. Alikazia hasa maswali ya afya ya uzazi na kupinga ukeketaji.[3]
Alishiriki kuandaa itifaki kupinga na hatua dhidi ya ukeketaji wa wanawake ambao ulipata kibali juni 2013 huko Navarra, Hispania.
Maandishi
haririMwaka 2015 alichapisha Indomable: de la mutilación a la vida (Indomitable: From Mutilation to Life), na Nyumba ya uchapaji ya Ediciones Península, ambayo alizungumza kuhusu maisha yake.[4]
Marejeo
hariri- ↑ Cervantes, Biblioteca Virtual Miguel de. "Obras de Djarra Sani, Fátima, 1968- - Pag. 1". www.cervantesvirtual.com. Iliwekwa mnamo 5 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Fátima Djarra Sani, mediadora de Médicos del Mundo, pregonera de la Navidad en Pamplona - Tribuna Feminista". tribunafeminista.org. 14 Desemba 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 5 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Fátima Djarra Sani: "Cada vez se practican más ablaciones a bebés"
- ↑ Imparcial, El. "Fátima Djarra Sani / Gorka Moreno: Indomable". elimparcial.es. Iliwekwa mnamo 5 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fátima Djarra Sani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |