Guinea Bisau

Guinea-Bisau (pia: Ginebisau) ni nchi ndogo katika Afrika ya Magharibi.

República da Guiné-Bissau
Jamhuri ya Guinea-Bissau
Bendera ya Guinea-Bissau Nembo ya Guinea-Bissau
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unidade, Luta, Progresso
(Kireno: Umoja, Mapambano, Maendeleo)
Wimbo wa taifa: Esta é a Nossa Pátria Bem Amada (Hii ni nchi yetu tunayoipenda)
Lokeshen ya Guinea-Bissau
Mji mkuu Bisau 1
11°52′ N 15°36′ W
Mji mkubwa nchini
Lugha rasmi Kireno
Serikali Jamhuri
Umaro Sissoco Embaló
Nuno Gomes Nabiam
Uhuru
kutoka Ureno
 - Ilitangazwa
24 Septemba 1973
 - Ilikubaliwa
10 Septemba 1974
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
36,125 km² (ya 136)
22.4
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 2002 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,693,398 (ya 148)
1,345,479
44.1/km² (ya 154)
Fedha Franki ya CFA (XAF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC+0)
(UTC)
Intaneti TLD .gw
Kodi ya simu +245

-

1Note: Rais (mstaafu)Kumba Ialá aliwahi kutangaza mji mkuu utahamishwa kwenda Buba lakini hakuna dalili za utekelezaji hadi sasa.


Map of Guinea-Bisau

Iko mwambaoni kwa Bahari Atlantiki ikipakana na Senegal upande wa kaskazini na Guinea upande wa kusini.

JiografiaEdit

Guinea-Bisau ni kati ya nchi ndogo sana za Afrika; takriban 22% ni visiwa na bahari. Sehemu ya bara ni tambarare. Funguvisiwa ya Bissagos yenye visiwa 77 iko karibu na pwani.

MijiEdit

Miji mikubwa zaidi ya Guinea Bisau ni: Bisau (wakazi 388.028), Bafatá (wakazi 22.521), Gabú (wakazi 14.430), Bissorã (wakazi 12.688), Bolama (wakazi 10.769) na Cacheu Einwohner (10.490).

HistoriaEdit

Zamani ilikuwa koloni la Ureno kwa jina la Guinea ya Kireno. Baada ya uhuru (1973/1974) jina la mji mkuu wake lilishika nafasi ya nchi tawala kuwa Guinea-Bisau kwa kusudi la kuitofautisha na nchi jirani ya Guinea na ile ya Guinea ya Ikweta.

WatuEdit

Wakazi walikuwa 1,515,000 mwaka 2010, wakati walikuwa 518,000 tu mwaka 1950.

MakabilaEdit

Waafrika ni 99%: makundi makubwa ni Wabalanta 30%, Wafulbe 20%, Wamanjaca 14%, Wamandinka 13%, Wapapel 7%). Wazungu na machotara chini ya 1%.

LughaEdit

Pamoja na lugha asilia, 14% za wakazi wanasema Kireno ambacho ndicho lugha rasmi na 44% wanatumia Krioli maalumu ya Kireno ambayo ni kama lugha ya taifa inayounganisha makabila.

DiniEdit

Takriban 50% ni Waislamu (hasa Wasuni), 40% wafuasi wa dini asilia za Kiafrika, 10 % Wakristo (hasa Wakatoliki).

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • Abdel Malek, K.,"Le processus d'accès à l'indépendance de la Guinée-Bissau.",In : Bulletin de l'Association des Anciens Elèves de l'Institut National de Langues et de Cultures Orientales, N°1, Avril 1998. – pp. 53–60
  • Forrest, Joshua B., Lineages of State Fragility. Rural Civil Society in Guinea-Bissau (Ohio University Press/James Currey Ltd., 2003)
  • Galli, Rosemary E, Guinea Bissau: Politics, Economics and Society, (Pinter Pub Ltd, 1987)
  • Lobban, Jr., Richard Andrew and Mendy, Peter Karibe, Historical Dictionary of the Republic of Guinea-Bissau, third edition (Scarecrow Press, 1997)
  • Vigh, Henrik, Navigating Terrains of War: Youth And Soldiering in Guinea-Bissau, (Berghahn Books, 2006)

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Biashara
Habari
Afya
Jiografia


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guinea Bisau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.