Fannu bint Umar ibn Yintan (alifariki mnamo mwaka 1147) alikua mtoto wa mfalme ambae alikua kama kamanda katika kipindi cha Almoravid, na alikua akivalia mavazi ya kiume. Alishiriki vita mbalimbali mojawapo ikiwa kuilinda ngome ya Marrakesh[1] katika mji wa Almohad mwaka 1147.[2]

Maisha

hariri

Alilelewa katika falme ya Almoravid Marrakesh kama mtoto wa kike wa Umar ibn Yintan. Akiwa kama mtoto wa mfalme alikua na heshima kubwa ukilinganisha na waislamu wengine Almoravid moroko. Wanawake wa falme walijulikana kuwa na ushawishi mkubwa katika maswala ya nchi kama ilivyokua tamaduni mfano Zaynab an Nafzawiyyah, alikua mwanzilishi wa nasaba.wanawake wa Moroko hawakuvaa mavazi yakufunuika vichwa na nyuso zao, na elimu kwa wanawake ni jambo lililopitishwa. mfano wa wanawake hao ni Hafsa Bint al hajj al Rukuniyya waliofundisha kozi mbalimbali kwenye falme hiyo na wanawake wengne kuwa madaktari.[3]

Marejeo

hariri
  1. Bennison, Amira K. (2016-07-05). Almoravid and Almohad Empires (kwa Kiingereza). Edinburgh University Press. ISBN 978-0-7486-4682-1.
  2. Bennison, Amira K. (2016-07-05). Almoravid and Almohad Empires (kwa Kiingereza). Edinburgh University Press. ISBN 978-0-7486-4682-1.
  3. "Fannu", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-04-20, iliwekwa mnamo 2024-09-28