Bunilizi ya kinjozi

(Elekezwa kutoka Fantasy)

Bunilizi ya kinjozi (au bunilizi ya kifantasia, kwa Kiingereza fantasy) ni utanzu fulani wa fasihi andishi. Katika bunilizi hiyo mwandishi anatumia matukio au wahusika wasio wa kawaida.

Mifano ya bunilizi ya kinjozi katika fasihi ya Kiingereza ni: "A Midsummer Night's Dream" (Ndoto ya Usiku Mmoja) ya William Shakespeare, "Gulliver's Travels" (Safari za Guliveri) ya Jonathan Swift, na "The Lord of the Rings" (Bwana wa Mapete) ya J.R.R. Tolkien.

Bunilizi ya kinjozi hutofautishwa na bunilizi ya kisayansi kwa vile haisifu mambo ya teknolojia bali inatumia maajabu na viumbe vya visasili.

Marejeo

hariri
  • Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.