Fasihi andishi

Fasihi andishi ni sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.

Ushairi wa sufi wa kifalsafa

Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi.

Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa hadithi fupi, riwaya, tamthiliya, insha, shairi n.k.

Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli.

Sifa za fasihi andishiEdit

  • Ni mali ya mtu binafsi
  • Hupitishwa kwa njia ya maandishi
  • Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
  • Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika uwasilishaji wake
  • Huweza kutunzwa kwa muda mrefu.

Dhima za fasihi andishiEdit

  • Kukuza lugha
  • Kuburudisha
  • Kuelimisha
  • Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi.

MarejeoEdit

  • Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fasihi andishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.