Farakano la Kanisa la Magharibi

(Elekezwa kutoka Farakano la magharibi)

Farakano la Kanisa la Magharibi lilitokea ndani ya Kanisa Katoliki katika miaka 1378-1418.

Ramani ikionyesha nchi zilizounga mkono Papa wa Avignon (nyekundu) au Papa wa Roma (buluu) wakati wa farakano la Magharibi; baadaye Mtaguso wa Pisa (1409) ulisababisha mlolongo wa tatu wa waliojidai kuwa Papa halisi.

Makardinali wenye jukumu la kumchagua Papa walichagua wawili, mmoja baada ya mwingine, na hivyo kusababisha isieleweke yupi ana haki ya kuongoza.

Siasa ilijiingiza na kudumisha fujo kubwa, ingawa si kuhusu mafundisho ya imani, mpaka Mtaguso wa Konstanz (14141418) ulipotoa suluhisho.

Hata hivyo ilibaki athari mbaya juu ya mamlaka ya Mapapa waliofuata.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • The Three Popes: An Account of the Great Schism, by Marzieh Gail.
  • The Great Schism: 1378, by John Holland Smith (New York 1970).
  • The Origins of the Great Schism: A study in fourteenth century ecclesiastical history, by Walter Ullmann (Hamden, Conn: Archon Books, 1967 (rev. of 1948 original publication)).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Farakano la Kanisa la Magharibi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.