Fatim-Zahra Ammor au Fatima-Zahra Ammor (amezaliwa mwaka 1967) ni mhandisi, mwanasiasa na mshauri kutokea Moroko[1]Tangu oktoba 7 mwaka 2021 amekua waziri wa utalii, kazi za mikono na uchumi wa jamii nchini Moroko.[2]

Maisha na Elimu

hariri

Fatim-Zahra Ammor alizaliwa mwaka 1967 katika familia ya wasomi mjini Rabat. Baba yake alikua mfanyakazi wa benki na mama yake alikua mwandishi wa vitabu. Baaada ya kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya Lycee Lyautey katika mji wa Casablanca, alienda moja kwa moja nchini Ufaransa kuendelea na masomo. Kisha akajiunga na shule maalumu ya mbinu endelevu katika mji wa Paris alipotunukiwa shahada ya uhandisi mnamo mwaka 1991.[3]

Marejeo

hariri
  1. "Maroc : une journée avec Fatim-Zahra Ammor, ministre « tout-terrain » du Tourisme - Jeune Afrique.com". JeuneAfrique.com (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
  2. "Qui est Fatim-Zahra Ammor, ministre du Tourisme, de l'Artisanat et de l'Economie sociale et solidaire ? | Challenge.ma". archive.challenge.ma. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
  3. https://snrtnews.com/fr/article/fatim-zahra-ammor-une-dg-%C3%A0-la-t%C3%AAte-du-minist%C3%A8re-du-tourisme