Bilula (pia tapu ya maji, koki; ing. tap, faucet) ni aina ya valvu inayomwezesha mtumiaji kufunga na kufungulia maji yanayotoka kwenye bomba. Mara nyingi ni kifaa cha metali, kama vile chuma au shaba nyeupe lakini kuna pia za plastiki. Inafungwa mwisho wa bomba pale ambako maji huhitajika, kama vile kwenye mabeseni ya kuoshea vyombo jikoni au kunawia mikono, bafuni na kadhalika.

Bilula ya shingo defu
Bilula
Bilula kwa ndani

Bilula inajulikana tangu karne nyingi; haijulikani zilibuniwa wapi na lini lakini kuna mifano ya Roma ya Kale iliyohifadhiwa.

Kuna bilula za aina nyingi ukizingatia rangi, urefu, umbo, idadi ya vidude za kufungia na kufungulia maji, uwezo wake wakuzunguka kuangalia upande tofauti tofauti na utenda kazi. Bilula zingine zina uwezo wa kuchanganya maji kutoka bomba mbili tofauti kama vile maji yakutoka bomba la maji moto na maji baridi ya kutoka bomba ya maji baridi ili kuipatia anayetumia maji yenye joto anayotaka. Pia kuna bilula za kidijiti zenye vihisio digitali za kufungulia na kufunga. Aina hizi za bilula hufungulia maji zenyewe punde tu mtu anapopitishia mkono karibu na kujifunga punde tu mtu anapotoa mikono.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.