Mkono

(Elekezwa kutoka Mikono)

Mkono ni kiungo cha mwili kinachoanza penye bega na kuishia penye kiganja na vidole. Huwa na sehemu mbili ambazo ni mkono wa juu na kigasha zinazounganishwa kwa kiwiko au kisugudi.

Sehemu za mkono

Mkono huishia kwa vidole vitano ambavyo ni: kidole gumba[1], kidole cha shahada, kidole cha kati, kidole cha pete na kidole cha mwisho. Vidole vyote huweza kufanya kazi pamoja.

Mifupa ya mkono wa kibinadamu

Miongoni mwa wanadamu, mkono ni kiungo kilichotokea kutokana na mabadiliko ya miguu ya mbele ya mamalia wengine. Mikono inafanya pia kazi muhimu katika lugha ya mwili na lugha ya ishara.

Tanbihi hariri

  1. Gumba ni kidole kifupi kinene cha kwanza
Sehemu za Mkono wa binadamu

Bega * Mkono wa juu * Kisugudi * Kigasha * Kiganja * Kidole gumba * Kidole cha shahada * Kidole cha kati * Kidole cha pete * Kidole cha mwisho


  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkono kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.