Open main menu


Chuma (kisayansi pia: feri kutoka Kilatini "ferrum") ni elementi na metali inayopatikana kwa wingi duniani. Kikemia ni elementi mpito yenye kifupi cha Fe na namba atomia 26 katika mfumo radidia.

Chuma (Feri)
Fe-TableImage.svg
Jina la Elementi Chuma (Feri)
Alama Fe
Namba atomia 26
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 55.845
Valensi 2, 8, 14, 2
Kiwango cha kuyeyuka 1811 K (1538 °C)
Kiwango cha kuchemka 3134 K (2861 °C)
Asilimia za ganda la dunia 4.7 %
Hali maada mango

Chuma ni kati ya metali muhimu sana duniani. Chuma ni msingi wa feleji (chuma cha pua) ambacho ni uti wa mgongo wa maendeleo ya kiteknolojia ya miaka 100 iliyopita. Asilimia 95 ya vifaa vote vya metali vinavyotengenezwa duniani ni chuma.

Udhaifu wa chuma na matumizi yake ni tabia yake ya kubadilika kuwa kutu.

Viungo vya NjeEdit