Faustine Ndugulile
Faustine Engelbert Ndugulile (31 Machi 1969 - 27 Novemba 2024) alikuwa mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.[1] Pia aliwahi kuwa waziri kwa nyakati tofauti [2].
Elimu
haririMnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu hichohicho. Alifanya kazi katika miradi mbalimbali ya afya barani Afrika na kuo utaalamu wake katika sekta ya afya.
Taaluma na Siasa
haririNdugulile alifanya kazi katika nyanja mbalimbali za tiba, afya ya umma, na siasa. Alianza kama daktari wa afya ya umma na kupanda kwenye nafasi za uongozi. Alifanya kazi kama Msaidizi Mkurugenzi wa Huduma za Uchunguzi katika Wizara ya Afya, ambapo aliongoza juhudi za kuboresha huduma za damu na uchunguzi wa magonjwa, na kuwa na mchango mkubwa katika programu za afya za kitaifa. Katika ngazi ya kimataifa, alifanya kazi kama Mshauri Mkazi nchini Afrika Kusini, akichangia katika usimamizi wa mifumo ya afya ya kanda na mipango ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko. Alianza siasa mwaka 2010 alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Kigamboni nafasi aliyoitumikia mpaka mauti ilipomkuta. Ndugulile aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Tanzania) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Oktoba 2017. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020, tarehe 5 Desemba 2020, katika Baraza la Mawaziri la pili la Magufuli, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, wizara mpya iliyozinduliwa.[3]
Uongozi wa WHO
haririMnamo Agosti 2024, Ndugulile aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO).[4] Ndugulile aliheshimika sana kwa uongozi wake na maono yake katika sekta ya afya ya umma. Uteuzi wake kama Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika ulikuwa ni mafanikio makubwa kwa Tanzania na bara la Afrika. Alipokea pongezi kutoka kwa viongozi, ikiwa ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, aliyempongeza kwa uwezo wake wa kushughulikia changamoto kubwa za afya zinazokabili Afrika.
Kifo
haririNdugulile alifariki dunia tarehe 27 Novemba 2024, akiwa na umri wa miaka 55, wakati akipokea matibabu nchini India kwa ugonjwa ambao haukutajwa hadharani. Alikuwa anatarajiwa kuanza rasmi jukumu lake katika WHO mnamo Februari 2025.[5] [6].
Marejeo
hariri- ↑ "Member of Parliament CV". Bunge la Tanzania. 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-03. Iliwekwa mnamo 2017-05-06.
{{cite web}}
: Text "imeandaliwa Mei 2017" ignored (help) - ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/huyu-ndiye-dk-faustine-ndungulile-4837816
- ↑ Kolumbia, Louis (2020-12-07). "Tanzania: Magufuli's Unveils His Cabinet 30 Days After Taking Oath". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-23.
- ↑ "Dr Faustine Engelbert Ndugulile of Tanzania nominated as next director for WHO African Region", World Health Organization, 2024-08-27
- ↑ "WHO Africa director-elect dies while receiving treatment in India", ABC News, 27 November 2024.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/dk-ndugulile-afariki-dunia-4837348
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Faustine Ndugulile kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |