Faustine Ndugulile

Faustine Engelbert Ndugulile (alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.[1] Pia ni naibu waziri wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii.

Faustine Ndugulile

Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa dawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. alifanya kazi katika hospitali ya Muhimbili kuanzia (2001-2004) kama mtaalam wa microbiolojia. [2]

MarejeoEdit

  1. Member of Parliament CV. Bunge la Tanzania (2010). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-11-03. Iliwekwa mnamo 2017-05-06.
  2. https://prabook.com/web/faustine_engelbert.ndugulile/428854#