Feza Tadei Kessy (anayejulikana kwa jina la Feza[1]; amezaliwa Agosti 24, 1988) ni mwimbaji kutoka Tanzania na mshiriki wa zamani wa Big Brother Africa msimu wa nane mwaka 2013.[2][3]

Feza Kessy
Jina la kuzaliwaFeza Tadei Kessy
Amezaliwa(1988-08-24)Agosti 24, 1988 (age 36)
Nairobi, Kenya
Kazi yake

Maisha ya awali

hariri

Feza alizaliwa jijini Nairobi Kenya na kukulia huko na wazazi wenye asili ya Kitanzania na anatoka katika familia ya watoto wa nne. Alisoma shule ya msingi na sekondari kwenye jiji la Nairobi na Arusha. Feza alichukua diploma yake ya Tehama nchini Tanzania, alikwenda mbali zaidi na kusomea shahada ya kwanza ya usimamizi wa biashara nchini Uingereza.

Feza alianza kazi yake kama mwanamitindo ni mrembo wa zamani, mwaka 2005, alitawazwa kuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala na Miss Tanzania Mshindi wa pili akiwa na umri wa miaka 17.[4] Feza aliachia wimbo wake wa kwanza, Amani ya Moyo, mwaka 2013, baadaye akatoa My Papa, wimbo ambao ulimfanya kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaokuja kwa kasi. Mwaka wa 2015 alijiunga na Panamusiq na kuombwa kushiriki kwenye wimbo wa Macky 2 Living my Life.

Mnamo Mei 14, 2021, Feza alitia saini mkataba wake mkubwa zaidi alipotangazwa kuwa msanii wa kwanza wa Kike wa DB Records, lebo ya rekodi inayomilikiwa na nyota wa Nigeria Oladapo Daniel Oyebanjo, anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii D’banj. Feza alitoa wimbo wake wa kwanza Bless Me kwenye DB Records.[5]

Diskografia

hariri
  • Sanuka Ft Chege
  • Kaa Kijanja Ft Nikki wa Pili
  • My Papa
  • Simple Ft Dammy Krane
  • Amani ya Moyo

Viungo vya Nje

hariri
  1. Feza: Youtube Archived 25 Juni 2020 at the Wayback Machine.
  2. Feza Kessy: Instagram

Marejeo

hariri
  1. https://www.musicinafrica.net/directory/feza-kessy
  2. "Tanzania: Feza Kessy - Flying Tanzania's Flag Hig". All Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2013-05-30.
  3. "Feza Kessy: Tanzanian exits Big Brother". Nation Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2013-08-17.
  4. "Was it a mere change of guard at Miss tanzania?". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-08-31.
  5. "D'Banj Spreads To Tanzania; DB Records' New Signee, Feza Kessy, Drops Debut Single, 'Bless Me'". Within Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-05-14.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Feza Kessy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.