Asili (kutoka neno la Kiarabu) ni chanzo cha jambo fulani. Kila kitu kina asili yake, hakuna kitu duniani au ulimwenguni jumla kisichokuwa na asili.

Kwa mfano, kadiri ya dini mbalimbali, asili kuu ya binadamu wote ni Mungu aliyewaumba, ingawa pia Adamu na Eva wanatazamwa kuwa asili ya wale wote waliozaliwa nao.