Kweche
Kweche mtama
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Jenasi: Euplectes
Swainson, 1829
Ngazi za chini

Spishi 17:

Kweche ni ndege wadogo wa jenasi Euplectes katika familia Ploceidae ambao wanatokea Afrika. Kuna makundi mawili ya kweche. Ndege wa kundi moja (bishops) ni wadogo kwa kulinganisha na madume wana mkia mfupi wakati wa kuzaa. Wakati huo rangi za madume ni nyeusi na nyekundu, machungwa au njano. Ndege wa kundi jingine (widowbirds) ni wakubwa zaidi na madume wana mkia mrefu wakati wa kuzaa. Wakati huo rangi za madume ni nyeusi kwa kiasi kikubwa pamoja na sehemu zenye rangi nyingi kama nyeupe, nyekundu na njano.

Ndege hawa hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda. Hulifuma tago lao kwa manyasi katikati ya matete. Matago yao hupatikana katika makundi. Dume hufanya mruko wa kukoga ili kubembeleza jike akitimua manyoya yake (bishops) au akitandaza mkia wake (widowbirds). Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi

hariri