Franco Luambo Makiadi

Mwana muzika wa kongo
(Elekezwa kutoka François Luambo Makiadi)

François Luambo Luanzo Makiadi (6 Julai 1938 – 12 Oktoba 1989) alikuwa mtu mashuhuri wa karne ya ishirini katika muziki wa Kikongo na muziki wa Afrika kwa ujumla. Hasa huitwa Franco Luambo au, kifupi, Franco.Alijulikana sana kwa uwezo wake wa kuumiliki muziki wa rumba. Alipewa jina la utani kama "Mchawi wa Gitaa" hasa kwa juhudi zake ya upigaji wa gitaa. Akiwa kama mwanzilishi wa bendi ya muziki wa jazz OK Jazz, huhesabiwa kama moja kati ya waanzilishi muziki wa Kikongo wa kisasa.

Franco Luambo Makiadi
François Luambo Makiadi
Jina la kuzaliwaFrançois Luambo Luanzo Makiadi
Pia anajulikana kamaFranco
Amezaliwa(1938-07-06)Julai 6, 1938
Sona Bata, Zaire
(siku hizi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
AmekufaOktoba 12, 1989 (umri 51)
Mont-Godinne, Mkoa wa Namur, Ubelgiji
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mpiga gitaa
AlaGuitar
Vocals
Miaka ya kazi1950-miaka ya-1980
Ameshirikiana naOK Jazz, TPOK Jazz

Miaka ya awali

hariri

Alizaliwa mnamo mwaka 1938 katika nchi ambayo awali ilijukana kama Kongo ya Kibelgiji. Mama yake alikuwa anafanya biasha katika soko moja huko mjini Ngiri-Ngiri, na hasa alikuwa anapiga hamonica na vyombo vingine ili kuvutia wateja.[1]

Mnamo mwaka wa 1955, Franco alianzishwa bendi iliyoitwa OK Bar (ilikuwa sehemu ya Baa). Mwaka uliofuata bendi ilibadilishwa iina na kuitwa OK Jazz kwa niaba ya shemu ilipoanzia.[2]

Miaka ya 1980

hariri

Mwaka wa 1980, Franco alipewa jina la Mwalimu Mkuu wa Muziki wa Kizairena serikali ya Mobutu, heshima ambayo ilipelekea aonekane miongoni mwa watu walioiletea matatizo rukuki hadi ikawa ombaomba. Maudhui ya nyimbo zake zikaanza kubadilika kinagaubaga katika kipindi hiki na kuwa nyimbo za kizalendo na kusifia mashabiki wa kitajiri.

Franco alitumbuiza mara moja tu Marekani mnamo 1983.[3]

Mwaka wa 1985, Franco alitoa kibao chake kikali mno, Mario, kwa kuwasema vijana wanaopenda majimama ili wawekwe kinyumba

Alikufa mnamo 1989, ikapelekea mapumziko ya siku nne nchini Zaire.[2]

Discografia

hariri
Wasanii wanaochangia
  • The Rough Guide to Congo Gold (2008, World Music Network)

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Al Angeloro (March 2005).
  2. 2.0 2.1 "Franco: biography". allmusic.
  3. Ted Giola.

Jisomee

hariri
  • Congo Colossus: Life and Legacy of Franco and OK Jazz by Graeme Ewens, Publisher: Buku P. (12 Oct 1994), ISBN 978-0-9523655-0-1
  • Gary Stewart (2000). Rumba on the River: A History of the Popular Music of the Two Congos. Verso. ISBN 1859843689. 

Viungo vya Nje

hariri