Francis Imbuga

Mwandishi wa Tamthilia wa Kenya

'’’Francis Imbuga’’’ anatambulika kama gwiji wa maswala ya uigizaji nchni Kenya . Kama mwandishi wa tamthilia,muigizaji na hakimu wa michezo ya kuigiza,amekuwa kipao mbele wa mswala ya ubunifu,haswa kwa waandishi wanaoibuka.

Historia na masomo

hariri

Francis Imbuga alizaliwa katika kijiji cha Wenyange , Maragoli Magharibi, Magharibi mwa Kenya mnamo tarehe 2 Februari mwaka wa 1947. Tamthilia zake ambazo nyingi huzingatia kuwepo kwa umoja na maridhiano katika familia za kitamaduni za Afrika zinatokana na yeye kulelewa na nyanya na babu zake katika eneo la Chavakali.Kwenye mahojiano ya mwaka wa 1986,alikiri kuwa ni malezi yake yaliyomjenga kimaisha na kisanaa.Densi.methali,heshima na urembo wa Kiafrika zilitiririka na kudhihirika kwenye tamthilia zake na pia maishani mwake.

Hatima ya jamii ya Waafrika ilyozungukwa na itikadi ngeni ndio ilokuwa dhamira na maudhui ya kazi za waandishi waanzilishi wa Afrika,kazi ambazo Imbuga alizisoma.Kazi za Ngugi wa Thiong'o kama vile Weep Not, Child (1964), The River Between (1965), na The Black Hermit (1968) zina maudhui makuu ya mabadiliko ya kihistoria ya Waafrika na mizozo inayotokana na kuwepo kwa Wazungu katika Afrika.. Imbuga alizisoma kazi hizi pamoja na za waandishi wengine kama vile Elvania Zirimu, Peter Nazareth, Jonathan Kariara,na Okot p'Bitek.

Imbuga alisomea swala la "The Techniques of Improvised Drama" kwa shahada yake ya Masters .Kwa udhamini wa UNESCO kati ya miaka za 1974 na 1975 ,alipata kuzuru Idara ya Uigizaji (Drama Department ) ya University College, Cardiff;Taasisi ya Masomo ya Kiafrika (Institute of African Studies) katika Chuo Kikuu cha Ghana, Legon; na Idara ya Sanaa ya Uigizaji (Department of Theatre Arts) katika Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria. Mwaka wa 1976, Imbuga aliteuliwa kama mkufunzi katika Idara ya Mawasiliano ya Elimu na Teknolijia (Department of Educational Communication and Technology) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Alihamia mwaka wa 1978 Chuo Kikuu cha Kenyatta, na kupanda ngazi hadi kuwa Mkufunzi Mkuu na kuteuliwa Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Kingereza (Department of Literature).

Tajriba yake kwenye uigizaji ilianzia katika Shule ya Upili ya Alliance, ambako mchezo wa kuigiza wake ulioitwa Omolo uliteuliwa kwenye fainali za Kenya National Schools' Drama Festival mwaka wa 1969. Akiwa mhusika mkuu,Imbuga aliteuliwa kuwa Muigizaji Bora wa Mwaka,na maravmoja akaanza kuandikia kituo cha televisheni cha Voice of Kenya-kwa sasa KBC- mchezo wa kuigiza endelezi wa "Omolo"

Imbuga alipata shahada ya digrii kwenye Elimu (bachelor of arts degree in education) katika Chuo Kikuu cha Nairobi.Akiwa chuoni (1970-1973), Imbuga aliiguza kwenye zaidi ya michezo ya kuigiza hamsini kwenye kipindi cha African Theatre kwenye runinga ya Voice of Kenya.

Kazi yake

hariri

Tamthilia tisa za Imbuga zilizochapishwa huigizwa kila mara na kazi zake hujadiliwa katika semina mbalimbali duniani. Tamthilia zake kama vile—Betrayal in the City (1976), The Successor (1979), Man of Kafira (1984), na Aminata (1988)—zimesomeshwa katika shule za sekondari na Vyuo mbalimbali katika Afrika Mashariki na Kati. Kwenye tamthilia zake,Imbuga hutumia ufasaha kwenye fasihi ya Kiluhya ambayo ni lugha yake,kusimulia maudhui yake.Kama mwanzilishi wa waandishi wa Afrika,yeye husisitiza umoja na hadhi uliokuwepo kabla ya kuja kwa mkoloni.Adui wake mkuu ni Mzungu,ambaye alikuja kuharibu ustaarabu huu wa Mwafrika. Tamthilia zake zilizochapishwa hadi sasa ni: 1. Kisses of Fate (1972)

2. The Fourth Trial (1972)

3. The Married Bachelor (1973)

4. Game of Silence (1977)

5. Betrayal in the City (1976)

6. The Successor (1979)

7. Man of Kafira (1984)

8. Aminata (1988)

Marejeo

hariri

1. http://www.bookrags.com/biography/francis-d-imbuga-dlb/