Fredinah Peyton

mwanamuziki wa Rap na Hip Hop kutoka nchini Tanzania

Fredinah Peyton (anajulikana na Watanzania wengi kwa jina la Rah P ambalo limetokana na herufi chache za jina lake) ni mwanamuziki wa Rap na Hip Hop kutoka nchini Tanzania.

Fredinah Peyton
Mwanamzuki Rah P
Mwanamzuki Rah P
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Rah P
Nchi Tanzania
Alizaliwa 1986 mkoa wa Shinyanga - Tanzania
Aina ya muziki Rap, Hip Hop
Kazi yake uimbaji
Miaka ya kazi 2003 -
Ameshirikiana na Mr Nice na Benjamin wa Mambo Jambo

Rah P alizaliwa mwaka 1986 mkoani Shinyanga akiwa mtoto wa pili kati ya watoto wanne wa mzee Peyton, akiwa amepatia elimu yake ya msingi nchini Kenya na kuhitimu kidato cha nne huko nchini Uganda, na kuendelea na A level huko huko nchini Uganda.

Maisha ya Muziki hariri

Mwanadada huyu asiyekuwa na historia kubwa katika ulimwengu wa muziki alianza kuimba baada ya kuwa mpenzi mkubwa wa wanamuziki wa kutoka nchini Marekani kama vile akina Mc Lyte,Queen Pen na Destiny Child, mara nyingi alikuwa akiigiza nyimbo za wanadada hawa na kuzicheza kwenye matamasha mbalimbali ya kishule jambo lililomuongezea umaarufu mkubwa huku mama yake mzazi akipinga vikali kitendo cha mwanae kujishughulisha na muziki akiwa shuleni lakini wakati huohuo akipata msukumo kutoka kwa Dada yake mkubwa Georgia.

Mwaka 2003 mwanzoni nyota ya kuwa mwanamuziki ilianza kung’ara baada ya kupata nafasi ya kuimba kwenye tamasha moja huko Butiama,Shinyanga huku kukiwa na Wanamuziki wengine kama wakina Mr Nice na Benjamin wa Mambo Jambo waliokuwa ziarani mkoani humo, baada ya hapo ndipo mama yake alipoanza kumruhusu kufanya muziki ila kwa masharti ya kumaliza shule kwanza au kufanya wakati wa kipindi cha likizo

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fredinah Peyton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.