Benjamin wa Mambo Jambo
Benjamin Sixtus Busungu (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Benjamin wa Mambo Jambo; alizaliwa tarehe 11 Novemba 1976) ni msanii mwimbaji wa Hip Hop, Dancehall, Afro-Beat, Afro-Pop na pia mtayarishaji wa rekodi kutoka nchini Tanzania.
Benjamin wa Mambo Jambo | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Benjamin Sixtus Busungu |
Pia anajulikana kama | Benjamin |
Amezaliwa | 11 Novemba 1976 |
Asili yake | Sengerema, Mwanza Tanzania |
Aina ya muziki | Hip hop Afro-Pop Dancehall Bongo Flava |
Kazi yake | Singer/Producer |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 2000 - hadi leo |
Studio | Mwamba Productions Mzuka Records FM Studio Kokwa Production Napol Music |
Ame/Wameshirikiana na | Dknob Saida Karoli Zola D Sharama Papii Kocha Baba Nyau MC Chichi Bella |
Tovuti | https://web.facebook.com/benjaminwamambojambo/
https://www.instagram.com/benjaminwamambojambo/ https://open.spotify.com/artist/2xoxvoZEXPiijYGCGi2jgr |
Awali alikuwa na kundi la Mambo Jambo, kundi ambalo lilikuwa linafanya muziki wa hip hop katika miaka ya 2001/2002.
Vibao vyake binafsi ni pamoja na: "Nimefulia", "My friend" na "Bang"[1] na "Mdundiko", na kuweza kushirikishwa katika baadhi ya nyimbo za bongo flava na albamu kadhaa. Vilevile amepiga video za muziki mbalimbali nchini Tanzania.
Maisha
haririBenjamin alizaliwa katika Hospitali ya Bombo mjini Tanga, Tanzania.
Ni mtoto wa nne kuzaliwa katika orodha ya watoto kumi wa Sixtus Busungu. Alianza elimu yake ya msingi katika mwaka wa 1985 hadi 1991, katika shule ya msingi Mtejeta, wilaya ya Mpwapwa, katika mkoa wa Dodoma, Tanzania.
Kisha akaenda kujiunga na Shule ya Sekondari ya Lake mjini Mwanza, Tanzania, kwa kidato cha kwanza hadi cha nne akiwa hukohuko Mwanza.
Baada ya hapo, akaelekea katika mafunzo ya sanaa katika Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo kuanzia 1998 hadi 2000.
Kwa sasa anasomea shahada ya utayarishaji wa filamu katika Chuocha AFDA kilichopo Cape Town, Afrika Kusini.
Vinginevyo, aliendelea na masomo ya ufundi wa kompyuta na uhandisi wa sauti katika Dar Computer, UDSM.
Marejeo
hariri- ↑ Bang ya Benjamini Mkono mpya wa Benja na Miikka Mwamba
Viungo vya nje
hariri- Mambo Jambo Ilihifadhiwa 31 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine. katika CDbaby.com
- Mambo Jambo Ilihifadhiwa 25 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine. katika Mwamba Productions.com
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Benjamin wa Mambo Jambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |