Fredrick Bundala
Fredrick Bundala (alizaliwa 1 Desemba 1982 ) ni mwandishi wa habari na mjasiriamali wa Tanzania.
Fredrick Bundala.jpg | |
Amezaliwa | Fredrick Bundala December 1, 1982 |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Majina mengine | Skywalker |
Anafahamika kwa | Uandishi, Utangazaji |
Kazi maarufu | Mwandishi |
Elimu | St. Augustine University |
Cheo | Mkurugenzi |
Asasi | Simulizi na Sauti |
Anajulikana kwa ajili ya | Mwandishi wa Habari |
Dini | Mkristo |
Mwenza | Baby Lachman (2012 - Mpaka sasa) |
Watoto | 2 |
Tovuti | https://sns.co.tz/ |
Ni Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Lerock Media Group inayo miliki luninga mtandao maarufu kwa jina la Simulizi na Sauti ambayo inapatikana katika Mitandao ya kijamii hasa YouTube. Pia ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya MindTap Tanzania Limited.
Maisha Yake
haririAlizaliwa mkoani Shinyanga nchini Tanzania na kukulia katika kijiji cha Ngudu, wilaya ya Kwimba katika mkoa wa Mwanza na katika kukua kwake alikuwa akipenda sana kusikiliza redio huku watangazaji kama Phina Mango wakiwa ni watu walio tia mafuta katika ari yake ya kutaka kuwa mwanahabari nguli.
Elimu
haririAlijiunga na Musoma High School mwaka 2000 na kusomea Mchepuo wa HGK (Historia, Geagrafia na Kiswahili). Mara baada ya Kumaliza kidato cha sita akajiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino cha mkoani Mwanza huku akisoma masomo ya Uandishi wa habari katika kiwango cha shahada[1].
Ajira
haririVictoria FM Musoma
Radio Free Africa
Bongo 5
Dizzim Online
Simulizi na Sauti
haririImekuwa ni moja kati ya vyombo vya habari pendwa nchini Tanzania vyenye kutoa habari zote za michezo, burudani na Habari muhimu. Kuanza kwake kulianza kwa kusua sua huku fredrick Bundala wakiwa bado wanajitafuta. Simulizi na sauti ilianza mwaka 2017 ikiwa na wafuatiliaji wachache walio penda kusikiliza simulizi na hadithi kutoka kwa mwandishi na mtangazaji Fredrick. Ni moja kati ya Luninga mtandao na chombo cha habari chenye kuaminika na chenye kupendwa na wengi.
Tuzo na Teuzi Mbalimbali
hariri- Best Media Personality of the Year - East Africa Arts Entertainment Awards, 2023
- Best Digital Journalist Award Iliyo tolewa na The Tanzania Digital Awards - May, 2024