Froot Loops
Froot Loops ni aina ya chakula cha kiamshakinywa kinachotayarishwa na kampuni ya Kellogg's na huuzwa katika nchi zifuatazo: India, Australia, Kanada, New Zealand, Marekani, Ujerumani, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kilatini. Chakula hiki huwa katika vipande vidogo vyenye umbo wa mviringo (hasa lile jina la "loops") na huwa katika rangi mbalimbali na mionjo mbalimbali ya matunda.
Historia
haririKellog's ilianzisha bidhaa za Froot Loops katika mwaka wa 1963. Hapo mwanzoni, kulikuwa na miviringo nyekundu,rangi ya machungwa na manjano,ya kijani kibichi iliongezwa baadaye , kisha zambarau na hatimaye ya samawati ikaongezwa pia.
Aina nyingine ya chakula hii inajulikana kama Froot Loops 1/3 Less Sugar, Marshmallow Froot Loops, na Froot Loops Smoothie.
Katuni ya kuwakilisha bidhaa hii katika matangazo ya televisheni ama kampeni ya bidhaa hii ni Toucan Sam.
Aina Mbalimbali
haririKellogg's imejaribu kupanua bidhaa ya aina ya Froot Loops kwa njia nyingi kwa mfano kwa kuunda Snack Ums. Snack Ums ilikuwa kama nafaka za kawaida za kuliwa kama kiamsha kinywa lakini kubwa zaidi. Kaulimbiu yao ilikuwa "Super sized bites with deliciously intense natural fruit flavors......Flavor bursting! ". Ikimaanisha kuwa ukila chakula hiki chenye mionjo mingi ya matunda, utahisi utamu sana!
Aina nyingine ya Froot Loops iliyoanzishwa na kampuni ya Kellog's ilikuwa Froot Loops Cereal Bar. Froot Loops Cereal Bar ilikuwa nafaka zilizoshikanishwa kwa vyakula vingine mbalimbali katikati ,juu na chini. Hata hivyo, bidhaa hii haikuwa na mafanikio huku maoni mengi ya watu kuwa haikuonja kama nafaka hata kidogo. Kaulimbiu yao ilikuwa "The goodness of cereal and milk!" hasa wakimaanisha "Uzuri wa nafaka na maziwa".
Utamaduni wa Pop
haririFroot Loops imehusishwa mara kadhaa katika kipindi cha televisheni cha All in the Family kama nafaka iliyopendwa sana na mhusika Archie Bunker.
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti Rasmi
- Froot Loops kwenye tovuti rasmi ya Kellog's Ilihifadhiwa 31 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.: Inahusisha habari kuhusu virutubishi na vyakula vilivyohusishwa katika kutayarisha Froot Loops.