Genevieve Nnaji

Muigizaji, Mzalishaji na Muongozaji wa filamu kutoka nchini Nigeria

Genevieve Nnaji (alizaliwa 3 Mei 1979 mjini Mbaise, Imo, Nigeria)[1] ni mwigizaji, mzalishaji na muongozaji wa filamu kutoka nchini Nigeria. Alishinda tuzo ya  Africa Movie Academy award akiwa muigizaji bora wa kike aliye kuwa kama muhusika mkuu, mwaka 2005, ikimfanya kuwa muigizaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo.

Genevieve Nnaji

Genevieve Nnaji akiwa katika muda wa chakula cha mchana kwenye studio ya masuala ya mavazi ya St. Genevieve mjini Lagos Nigeria, Mei 2008
Amezaliwa Genevieve Nnaji
3 Mei 1979 (1979-05-03) (umri 45)
Mbaise, Imo, Nigeria
Kazi yake Mwigizaji, Mwanamitindo, Mwimbaji


Maisha ya awali

hariri

Nnaji alizaliwa Mbaise, jimbo la Imo, Nigeria, na alikulia  Lagos. Akiwa wa nne kati ya watoto nane, alikulia katika familia ya maisha ya kati; baba yake alifanya kazi kama mhandisi na mama yake alifanya kazi kama mwalimu wa shule ya awali. Alisoma katika chuo cha  kimethodist cha  wasichana (Yaba, Lagos), kabla ya kuhamia chuo kikuu cha Lagos, ambapo alihitimu na shahada ya Sanaa ya ubunifu. Wakati akiwa chuoni alianza kutafuta kazi za uigizaji Nollywood.

Shughuli

hariri

Nnaji alianza shughuli zake za uigizaji akiwa kama mwigizaji mtoto kwenye tamthilia za televisheni – Ripples akiwa na umri wa miaka 8. Pia amewahi kushirikishwa kwenye matangazo ya biashara kadhaa ikiwemo kinywaji cha Pronto na sabuni ya Omo. Mnamo mwaka wa 1998 akiwa na umri wa miaka 19 alianza kuonekana katika soko la filamu za watu wakubwa za Kinigeria – “Most Wanted”.

Filamu zake za baadaye ni pamoja na Last Party, Mark of the Beast na Ijele.

Nnaji amepokea tuzo kadhaa kwa ajili ya kazi yake. Tuzzo hizo ni pamoja na kuopewa na jina la mwigizaji bora wa mwaka wa 2001 na City People Awards, na kupkea heshima ya kuwa mwigizaji bora mnamo mwaka wa 2005 kwenye African Movie Academy Awards (AMAA).

Mnamo mwaka wa 2004 ameingia mkataba na studio ya Kighana na kutoa albamu. Mnamo mwaka wa 2008, Nnaji ameanzisha mradi wa mavazi, "St. Genevieve," ambao pia huchangia asilia kadhaa katika mradi wa maendeleo ya uhisani.

Filmografia

hariri

  • 30 Days
  • Above Death: In God We Trust
  • Above the Law
  • Agbako
  • Age Of My Agony
  • Agony
  • Battleline
  • Blood Sisters
  • Break Up
  • Broken Tears - (akiwa na Van Vicker, Kate Henshaw-Nuttal na Grace Amah)
  • Bumper To Bumper
  • Butterfly
  • By His Grace
  • Camouflage
  • Caught In The Act
  • Church Business
  • Confidence
  • Could This Be Love
  • Critical Decision
  • Dangerous Sisters
  • Day of Doom
  • Deadly Mistake
  • Death Warrant
  • Emergency Wedding
  • Emerald
  • For Better For Worse
  • Formidable Force
  • Games Women Play
  • Girls Cot
  • Goodbye Newyork
  • God Loves Prostitutes
  • He Lives In Me
  • Honey
  • Ijele
  • Into Temptation
  • Jack Knife
  • Jealous Lovers
  • Keeping Faith

  • Last Weekend
  • Late Marriage
  • Letter to a Stranger
  • Love
  • Love Affair
  • Love Boat
  • Man of Power
  • More Than Sisters
  • Never Die For Love
  • Not Man Enough
  • Passion And Pain
  • Passions
  • Player
  • Power Of Love
  • Power Play
  • Private Sin
  • Prophecy
  • Rip Off
  • Rising Sun
  • Runs
  • Secret Evil
  • Sharon Stone
  • Sharon Stone In Abuja
  • Stand By Me
  • Super Love
  • Sympathy
  • The Chosen One
  • The Coming of Amobi
  • The Rich Also Cry
  • The Wind
  • Treasure
  • Two Together
  • U Or Never
  • Unbreakable
  • Valentino
  • Warrior's Heart
  • Women Affair

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Genevieve Nnaji kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.