Geofrey Kusuro
Geofrey Kusuro (alizaliwa Mutishet, 12 Februari 1989) ni mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Uganda.[1] Alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya mwaka 2008 katika mbio za mita 5000 za wanaume, bila kufika fainali. Katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya mwaka 2012, alishiriki katika mbio za mita 5000 za Wanaume, akimaliza jumla ya 37 katika Raundi ya 1, na kushindwa kufuzu kwa fainali..[2] Pia aliiwakilisha Uganda katika Mashindano ya Dunia mwaka 2009 na 2011.[3]
Alishinda Mashindano ya Dunia ya Mbio za Milima mwaka 2009, hivyo akawa Muganda wa kwanza kushinda taji hilo.[4]
Mwaka 2023, alishinda Madrid Marathoni kwa muda wa 2:10:29.[5]
Marejeo
hariri- ↑ Geoffrey Kusuro Archived Novemba 21, 2015, at the Wayback Machine. Sports Reference. Retrieved on 2015-04-26.
- ↑ "Geoffrey Kusuro Bio, Stats, and Results". Olympics at Sports-Reference.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-18. Iliwekwa mnamo 2017-11-26.
- ↑ "IAAF: Geofrey Kusuro | Profile". iaaf.org. Iliwekwa mnamo 2017-11-26.
- ↑ "IAAF: Geofrey Kusuro | Profile". iaaf.org. Iliwekwa mnamo 2017-11-26.
- ↑ "MYLAPS Sporthive Event Results". results.sporthive.com. Iliwekwa mnamo 2024-03-13.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Geofrey Kusuro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |