Georg von Hevesy
Georg Charles de Hevesy (1 Agosti 1885 – 5 Julai 1966) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Hungaria. Alifanya kazi katika nchi mbalimbali, kwa mfano Uingereza, Ujerumani na Uswidi. Hasa alichunguza isotopi. Mwaka wa 1923 aligundua elementi ya hafnium. Mwaka wa 1943 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Georg von Hevesy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |