George Lucas
George Walton Lucas, Jr. (amezaliwa tar. 14 Mei 1944 mjini Modesto, California) ni mwongozaji, mtayarishaji na mwandikaji wa script wa filamu wa Kimarekani. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kutayarisha mfululizo wa filamu za Star Wars na mfululizo wa filamu za Indiana Jones.
George Lucas | |
---|---|
George Lucas, mnamo 2009. | |
Amezaliwa | George Walton Lucas, Jr. Mei 14 1944 Modesto, California, Marekani |
Kazi yake | Mwongozaji, mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 1965-hadi leo |
Ndoa | Marcia Griffin (1969-1983) Mellody Hobson (2013) |
Watoto | 4 |
Lucas pia aliongoza filamu za THX 1138 (1970) na American Graffiti (1973). Akiwa pamoja na rafiki yake wa karibu Bw. Steven Spielberg, walifanikisha kutengenezwa kwa mfululizo wa filamu za Indiana Jones. Lucas vilevile ni mtaalam wa kuweka vionjo mbalimbali vya bunilizi ya kisayansi, na pia ameanzisha kampuni yake inayoandaa mambo mengi yahusianayo na filamu na kadharika. Alikuwa mwandishi sugu na aliyeshamiri katika uwanja wa uigizaji (sonkolimike@gmail.com).
Viungo vya nje
hariri- George Lucas at the Internet Movie Database
- George Lucas katika the Notable Names Database
- Lucas bio page Ilihifadhiwa 5 Aprili 2004 kwenye Wayback Machine. at Lucasfilm.com
- Star Wars: George Lucas
- [1] Ilihifadhiwa 17 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine. Viewable Clips from Lucas' student films
- [2] Ilihifadhiwa 3 Februari 2008 kwenye Wayback Machine. George Lucas Plaza
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu George Lucas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |