Gesi miminika
Gesi miminika (kwa Kiingereza: liquefied natural gas; kifupi: LNG) ni gesi asilia katika hali ya kiowevu au miminika. Ni dutu safi isiyo na rangi na isiyo na sumu,[1] inayotengenezwa kwa kupoza gesi asilia hadi nyuzi joto -160ºC hadi kiwango ambacho inakuwa kimiminika. Mchakato huo hurahisisha usafirishaji wenye ufanisi wa gesi asilia kwa kutumia barabara (malori) au bahari (meli).[2] Sababu kuu ya kupoza gesi ni, gesi miminika ina ujazo mdogo mara 600 kuliko gesi asilia ikiwa katika hali ya kawaida.[3]
Uzalishaji
haririAsilimia kubwa ya gesi asilia hukatama kwenye chanzo na kusafirishwa kwa njia ya bomba baada ya kuisafisha hadi kufikia hali ya methani safi kiasi[4]. Pasipo mabomba ni muhimu kupunguza ujazo wa gesi hii ili kuisafirisha ama kwa meli au kwa malori.[5]
Hadi mwaka 2012, duniani kote kulikuwa na vituo 20 vya kuzalisha na kusafirisha nje gesi miminika, vituo 63 vya kuingiza gesi miminika ndani ya nchi, na takriban meli 300 za kubeba gesi ya kimiminika zote zikiwa na uwezo wa kubeba tani za meta milioni 750 za gesi ya kimiminika kila mwaka. Kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka sana kwa kipindi cha miaka kumi ijayo kutokana na umaarufu unaoongezeka wa chanzo hicho safi cha kuwashia moto.[6]
Uchumi
haririUjengaji wa mitambo ya gesi miminika unahitaji mtaji mkubwa na yenye madeni makubwa.[7] Lakini wakati gesi miminika ina gharama kiasi kuizalisha, maendeleo ya teknolojia yanapunguza gharama hizo zinazotokana na kuifanya kimiminika na kuirudisha tena katika hali yake ya gesi asilia.[8] Chapisho la BP World Energy Outlook lilitabiri mnamo mwaka 2012 kwamba biashara ya gesi miminika itakua kwa haraka maradufu kama ulivyokua haraka uzalishaji wa gesi asilia duniani, yaani kwa kiwango cha asilimia 4.4 kwa mwaka.[9]
Marejeo
hariri- ↑ "Focus on LNG" Naturalgas.org, iliangaliwa 2019
- ↑ "What is LNG Ilihifadhiwa 4 Januari 2019 kwenye Wayback Machine." Center for Liquified Natural Gas, iliangaliwa Juni 2019
- ↑ "Liquified Natural Gas (LNG Ilihifadhiwa 30 Januari 2014 kwenye Wayback Machine." NaturalGas.org, retrieved 13 February 2012.
- ↑ The Transportation of Natural Gas Naturalgas.org, iliangaliwa 2019
- ↑ "Overview-About LNG Ilihifadhiwa 18 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine." Center for Liquified Natural Gas, retrieved 13 February 2012.
- ↑ "What is LNG? Ilihifadhiwa 31 Desemba 2011 kwenye Wayback Machine." ConocoPhillips, retrieved 13 February 2012.
- ↑ "Analysis: East Africa risks missing LNG boom Ilihifadhiwa 18 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine." Reuters, 19 September 2012.
- ↑ "Liquified Natural Gas (LNG Ilihifadhiwa 30 Januari 2014 kwenye Wayback Machine." NaturalGas.org, retrieved 13 February 2012.
- ↑ "World Energy Outlook 2030 Ilihifadhiwa 11 Machi 2014 kwenye Wayback Machine." BP, retrieved 13 February 2012.