Bahari ni eneo kubwa lenye maji ya chumvi. Katika Kiswahili cha kila siku neno hili hutumiwa pia kwa kutaja magimba madogo zaidi ya maji kama vile ziwa.

Bahari na visiwa.

Kwa maana ya kijiografia bahari hasa ni bahari kuu ya dunia (kwa Kiingereza ocean) yaani maeneo makubwa ya maji ya chumvi ambayo ni kama gimba moja. Bahari kuu ya dunia inafunika asilimia 71 za uso wa dunia.

Katika matumizi ya kawaida, neno "bahari" humaanisha pia eneo la pekee ambalo ni sehemu ya bahari kuu inayogawiwa na mabara katika pande tatu kubwa:

Wataalamu mara nyingi huhesabu maeneo karibu na ncha ya kaskazini na ncha ya kusini ya dunia kama bahari kubwa ya nne na ya tano yaani

Tena neno "bahari" linatumika pia kwa maeneo ambayo ni bahari za pembeni za bahari tatu kubwa kama vile Mediteranea, Baltiki.

Bahari ni muhimu sana kwa ajili ya maisha na hali ya hewa duniani. Bahari zinashika asilimia 96.5 za maji yote ya dunia. Maji ya bahari yana takriban asilimia 3.5 za chumvi ndani yake. Kiwango hiki hutofautiana kidogo katika sehemu mbalimbali: kutokana na uvukizaji mkubwa penye joto kwa matumizi ya binadamu hata kwa matumizi ya mimea na wanyama wa nchi kavu haifai. Lakini bahari pia ni chanzo cha mvua kwa sababu mawingu hutokea hasa juu ya bahari. Katika mwendo wa uvukizaji, chumvi inabaki na mvuke unapaa bila chumvi ndani yake kuwa mawingu na kurudi katika mwendo wa usimbishaji. Usimbishaji unaleta maji yanayojaza mito na maziwa hata akiba za maji chini ya ardhi.

Tangu zamani bahari ni njia kuu za mawasiliano ya kimataifa. Hadi leo asilimia 92 ya mizigo yote hubebwa kwa meli baharini kati ya bandari.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: