Barabara ni njia iliyotengenezwa ili kupitisha binadamu akitumia vyombo vya usafiri kama vile magari, pikipiki, baiskeli pamoja na farasi.

Baraste kuu huwa na njia zilizotengwa kwa kupunguza hatari ya ajali
Barabara nyingi katika Afrika bado hazina lami zikihitaji matengenezo za mara kwa mara hasa baada ya mvua
Barabara ya Roma ya Kale huko Pompei, Italia.

Lengo ni kurahisisha mawasiliano toka mahali hadi mahali, hivyo ni kati ya miundombinu muhimu zaidi.

Huko Misri barabara za kwanza zilitengenezwa miaka 2,200-2,600 iliyopita,[1] lakini ziliwahi kuwepo za miaka 4,000 KK huko Ur, Iraq.

Barabara kuu

hariri

Mara nyingi barabara kuu hutumika kupitishia magari makubwa lakini na madogo na matumizi ya wanadamu pamoja na vyombo mbalimbali hususani vinavyomhusu mwanadamu. Mara chache barabara kuu hupitiwa na wanyama.

Barabara hizo huweza kuunganisha nchi na nchi, kwa mfano Tanzania na Kenya.

Mara nyingi barabara kuu husaidia kuinua uchumi wa nchi husika na nchi jirani ambayo imeunganishwa na barabara hiyo kwa kupitisha bidhaa mbalimbali, wakiwemo wanyama na wanadamu, na kwa namna moja au nyingine huinua nchi hizo hata kijamii na kimaendeleo kwa ujumla.

Barabara za pekee kwa matumizi ya usafiri wa haraka wa magari mengi zinajengwa kwa kutumia njia za pekee zinazotengwa kwa kila mwelekeo na bila mikingamano huitwa baraste kuu. Baraste kuu ya kwanza katika Afrika ya Mashariki ilitengenezwa nchini Kenya kati ya Nairobi na Thika.

Barabara ya mchipuko

hariri

Barabara ya mchipuko ni barabara ambayo hutumiwa mara chache endapo kama barabara kuu itakuwa na matengenezo. Barabara hii hurahisisha mawasiliano kati ya barabara kuu, hivyo hupunguza msongamano wa magari, hususani katika miji mikubwa.

Ubora wa barabara

hariri

Ni ile hadhi ya bararabara iliyoundwa au kutengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ili barabara iweze kukaa kwa muda mrefu na kwa ubora uleule kama mwanzo,

Sasa katika bara la Afrika barabara zinahitajika ziwe kwa kiwango kikubwa katika maeneo ambayo nchi kama nchi hutegemea hapo k.mf. viwanda.

Barabara ili iwe bora inahitajika kuwa na lami, pia iwe na alama za barabarani na pia inahitaji kutunzwa, k.mf. kufanyiwa usafi mara kwa mara na tena ukarabati wa mara kwa mara.

Tunatakiwa tuziboreshe barabara zetu ili tupite kwa urahisi, pia tuepukane na ajali mbaya za barabarani.

Pia tunatakiwa tutunze barabara zetu kimandhari ili ziwe safi kwa watumiaji na hao watumiaji wasitupe taka ovyo kwa sababu endapo taka zitatupwa ovyo husababisha uchafuzi katika barabara.

Lami ni mabaki ya mafuta yaliyosafishwa yenye rangi nyeusi; kwa maneno mengine ni madini yanayonata sana na hutumika kujengea barabara au kutia kwenye vyombo vya baharini ili maji yasipenye.

Katika ulimwengu wa sasa maeneo mengi duniani yamekuwa yakitegemea huduma hii muhimu, ila barabara za lami zimekuwa zikipata changamoto nyingi za kimazingira pindi zinapotengenezwa.

Nini hufanya barabara za lami kuharibika?

hariri

Kuna vitu vingi vya kuangalia ukiwa unarekebisha [2] njia za miguu au barabara kuu. Kwanza, tafuta sababu ya kuharibika. Sababu mbili kuu za kuharibika ni

  • mionzi ya jua na
  • maji[3].

Mionzi ya jua huharibu barabara, inayopoelekea barabara kuwa na mivunjiko. Maji hupenya kwenye mivunjiko na hufanya maligafi muhimu kuzimuliwa na kuchujwa. Malighafi huwa yakitolewa kutoka chini katika barabara ya lami, na hufanya lami kuharibika na kuwa shimo. Baada ya shimo kutokea, sehemu ya chini inabidi itengenezwe kabla haijatumiwa. 

Kwanza kabisa, inatakiwa utoe malighafi zote zilizozimuliwa. Ukubwa wa mtambo wa kuchimbia utategemea na eneo lililoharibika. Malighafi yanaweza kutolewa na kitu chochote  kuanzia mitambo mdogo hadi mitambo mikubwa kabisa.

Baada ya kuchunguza eneo, ni muhimu kukata kipenyo cha eneo husika. Chora kwa mistari kwanza na chaki ukiwa na vifaa vya kupimia. Mistari hii itafuatiwaa na chaki kubwa itakayoonyesha mistari iliyonyooka ikifuata kipenyo cha eneo la tatizo.

Kwa kumaliza hizi hatua mwanzo, matokeo yatakayokamilika yatakuwa imara na yenye mwonekano mnzuri. Baada ya kukata hilo eneo, kwa uangalifu ondoa lami na malighafi zingine kwenye eneo lililo athirika. Eneo linatakiwa kuwa safi na vipunje punje. Malighafi yenye unyevu yanatakiwa kutolewa katika mji ili kuweza kuleta uimara wa eneo jipya lililotengenezwa.

Baada ya kuondoa malighafi zenye unyevu, Bandika eneo husika kwa mawe, shindia na fukia. Kulingana na eneo lililo chimbwa, ili kubana malighafi mpya vizuri ukiwa unaweka malighafi. Baada ya kutitia malighafi, mipako ya kuwambisha inabidi iwekwe. Mipako inabidi iweke vizuri ili kuunganisha eneo la chini na mchoro mpya.

Madhara ya ajali

hariri

Ajali za barabarani husababisha nguvu kazi ya taifa kupungua; mfano: kupoteza maisha,ulemavu wa kudumu, pia huchangia kupungua kwa maendeleo hata ya nchi.

Pia katika jamii huleta matatizo mengi na hasara kwa ujumla kutokana na kutumika gharama nyingi wakati wa matibabu na hivyo kupoteza pato la jamii kwa ujumla kutokana na kutumia fedha ili kuwatibu walioathirika na ajali hizo.

Tanbihi

hariri
  1. John Noble Wildord. "World's Oldest Paved Road Found in Egypt", New York Times. Retrieved on 2012-02-11. 
  2. "Concrete Sidewalk, Driveway Repair Contractor, Brooklyn". www.sidewalkrepairsbrooklyn.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-27. Iliwekwa mnamo 2019-06-19.
  3. Barabara ya lami yayeyushwa na jua kali Australia (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-07-05, iliwekwa mnamo 2019-06-19
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barabara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.