Giuliano Gemma (2 Septemba 1938 - 1 Oktoba 2013) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Italia, aliyewahi kuwika katika filamu za western ya Italia, maarufu kama spaghetti western.

Giuliano Gemma

Maisha ya Mwanzo na Filamu Edit

Gemma alizaliwa mjini Rome, Italia. Awali alikuwa akifanya kazi kama mtu wa kucheza sehemu za hatari katika filamu (Stuntman) kisha akapewa ofa ya kuigiza, na muongozaji wa filamu za kitaliana bwana "Duccio Tessari", ambaye pia alikuwa nyota wa filamu ya Arrivano i titani ya mwaka (1962).

Gemma pia aliwahi kuonekana katika filamu ya Luchino Visconti Il Gattopardo. Baadae Gemma akaenda kuwa nyota wa filamu za spaghetti westerns, ambako ndiko alikopata mafanikio makubwa kabisa, kwa kucheza kama shujaa katika filamu kama vile A Pistol for Ringo au (Una pistola per Ringo), Blood for a Silver Dollar au (Un dollaro bucato) na Day of Anger au (I giorni dell'ira).

Giuliano mpaka leo hii bado anafanya shughuli zake katika televisheni moja hivi ya nchini Italia. Ingawaje anaoneka kama bado ni mwigizaji wa filamu za western, nchini Italia. Gemma alicheza filamu nyingi sana, ikiwemo ile ya muongozaji "Valerio Zurlini, iliitwa Il deserto dei tartari pia alicheza katika filamu ndogo ndogo, ikiwemo Luchino Visconti, alitumia jina la "Garibaldi General", pia akatumia jina la masterpiece, katika filamu ya Il Gattopardo.

Gemma pia ana binti yake aitwae Vera Gemma, nae pia mwigizaji. Giuliano Gemma pia mchongaji wa masanamu.

Filamu Alizocheza Gemma Edit

 • Arrangiatevi! (1959)
 • Il Gattopardo (1963)
 • Angelica (1964)
 • Una pistola per Ringo (1964)
 • Adiós gringo (1965)
 • Angelica alla corte del re (1965)
 • Un dollaro bucato (1965)
 • I lunghi giorni della vendetta (1966)
 • Per pochi dollari ancora (1967)
 • I giorni dell'ira (1968)
 • Anche gli angeli mangiano fagioli (1973)
 • Il deserto dei Tartari (1976)
 • Il prefetto di ferro (1977)
 • Sella d'argento (1978)
 • Tenebrae (1982)
 • Tex e il signore degli abissi (1985)
 • Speriamo che sia femmina (1986)
 • La donna del delitto (2000)

Ona Pia Edit

Viungo vya Nje Edit