Gladness Deogratias

Gladness Deogratias ni Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB nchini Tanzania. [1]

Gladness Deogratias
Nchi Tanzania
Majina mengine Gladness
Kazi yake Amesomea Masuala ya Biashara
Mwajiri Benki ya NMB
Cheo Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB
Dini Mkristo
Ndoa Ameolewa
Watoto 3
Mahusiano Ni mke wa watoto watatuElimuEdit

Gladness alipata elimu ya shule ya msingi mkoa wa Dar es salaam katika Shule ya Msingi Chang’ombe na kuhitimu darasa la saba mwaka 1966. Baadaye alijiunga na Shule ya Sekondari Kifungilo na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2000. Baada ya kuhitimu Elimu ya Sekondari alifanikiwa kupata nafasi ya ufadhili wa masomo kupitia International School of Tanganyika [2] na kujifunza masomo ya Saikolojia. Mwaka 2006 Alihitimu shahada ya Sanaa katika  Usimamizi wa Masuala ya Fedha  Chuo Kikuu cha Nottimghan huko Nottimghan, Uingereza. Alihitimu Shahada ya pili ya Usimamizi wa biashara mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Oxford Brookes huko Oxford, Uingereza.


TaalumaEdit

Baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 2006 aliomba kufanya kazi katika benki ya LEHAM International European Bank ambapo alidumu kwa muda wa miaka miwili kisha kuamua kurudi nyumbani kwao Tanzania baada ya kutokea kwa mtikisiko wa Dunia kiuchumi uliopelekea kufungwa kwa benki hiyo. Baada ya kurejea Tanzania Gladness alianza kufanya kazi katika benki ya ABC kisha kuhamia benki ya NMB akifanya kazi kama Mkuu wa Biashara na baadae kupandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki hiyo ya NMB, Cheo alichodumu nacho hadi sasa [3]. Akiwa mfanyakazi wa NMB Gladness amekuwa mstari wa mbele katika kuleta chachu ya usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume katika benki hiyo.[4]

FamiliaEdit

Gladness Deogratias ameolewa na kubahatika kupata watoto watatu ambapo mtoto mmoja ni wa kike na wawili ni wa kiume Quinlan na Quintrell.

MarejeoEdit


  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gladness Deogratias kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.