Glamour
'Glamour ni jina la filamu iliyotoka mwaka 2011 kutoka nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Eva Issack, Bond Bin Suleiman, Tekila Mjata, Mustafa Hassanali, Edward Chogula. Imeongozwa na Amitabh Aurora na kutayarishwa na Javed Jafferji. Filamu inahusu masuala ya urembo na uanamitindo. Hasa kule kuwa na nia ya dhati juu ya kile unachokiamini na mwishowe kufanikiwa. Filamu inamzungumzia Sophia binti aliyelelewa katika mazingira ya dini ya Kiislamu na baadaye kujihusisha na masuala ya urembo ilhali malezi yake yanamkataza. Anapitia mazogo kadha wa kadha, hatimaye anafanikiwa katika nia yake ya kuwa mrembo mashuhuri. [1][2] Pamoja na mafanikio hayo, bado alijiona yeye bora zaidi na kujiingiza katika anasa za maisha zilizopelekea kuishia pabaya.[3]
Glamour | |
---|---|
Posta ya Glamour | |
Imeongozwa na | Amitabh Aurora |
Imetayarishwa na | Javed Jafferji |
Nyota | Eva Issack Bond Bin Suleiman Tekla Mjata Mustafa Hassanali Edward Chogula |
Imetolewa tar. | 3 Novemba, 2011 |
Ina muda wa dk. | 86 |
Nchi | Tanzania |
Lugha | Kiswahili |
Hadithi
haririSophie ni binti wa Kizanzibari aliyekuzwa katika mazingira yenye misingi mizuri ya dini ya Kiislamu ambaye siku zote alivaa vazi rasmi kwa wanawake ama binti wa Kiisilamu la hijab. Katika maisha yake hajapatapo kuwahi kuona wala kuwa na hata nakala moja ya picha yake kutoka na hali kuwa si nzuri kimaisha katika familia yake yote kiujumla. Siku moja mtaani tu anapigwa picha na mgeni mtalii aliyekwenda kutembea kisiwani Zanzibar.
Sophia alipoiona picha hiyo kwa mara ya kwanza tu alipenda. Hali hii ilimtia hamasa ya kutaka kupiga picha maishani mwake mote na hata kuonelea awe mwanamitindo kama kina Naomi Campbell ambao awali alikuwa akiwaona katika televisheni. Azimio hili lilileta ukakasi kwa mama yake mzazi, hakupendezewa nalo na kukataa katakata bintiye kutofanya maamuzi hayo. Lakini bahati mbaya mama anafariki dunia na binti anajikuta hakuwa wa kumsimamia wala kumkanya, ndipo anapoazimia kwenda jijini Dar es Salaam na kumtafuta mmoja ya wasimamizi wakubwa wa wanamitndo jijini huko Mustafa Hassanali.
Akiwa huko, alifanikiwa kupokelewa vizuri na wakala huyo, lakini baadaye analewa sifa na kujikuta anaacha kufuatilia kilichompeleka kujawa na anasa za maisha hali iliyopeleka kupata mazito katika maisha.
Washiriki
hariri- Eva Issack
- Bond Bin Suleiman
- Tekla Mjata
- Mustafa Hassanali
- Edward Chogula
Marejeo
hariri- ↑ Glamour Ilihifadhiwa 8 Januari 2017 kwenye Wayback Machine. katika Bongo Cinema.com
- ↑ Glamour katika Bongo Film Database - Blogu.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-24. Iliwekwa mnamo 2017-09-15. katika Bongo Celebrity Blogu
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Glamour kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |